25.3 C
Dar es Salaam
Monday, January 17, 2022

Uturuki yakasirishwa ufunguzi msikiti wa Hagia Sophia

ANKARA, UTURUKI

WIZARA ya Mambo ya Nje ya Uturuki imelaani taarifa za maofisa wakuu wa Ugiriki na maandamano yaliofanywa nchini humo baada ya waislamu kufanya sala katika jengo maarufu la Haggia Sophia. 

Sala hiyo ya Ijumaa ilifanyika juzi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miongo tisa.

Msemaji wa wizara hiyo Hami Aksoy amesema kwa mara nyingine Ugiriki imeonyesha pingamizi kali dhidi ya uislamu na Uturuki kwa kisingizio cha kukasirishwa na hatua za kufunguliwa msikiti huo wa Hagia Sophia kwa ajili ya kuendesha sala.

 Wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya kudumishwa kwa demokrasia nchini Ugiriki, waziri mkuu wa nchi hiyo Kyriakos Mitsotakis aliitaja hatua ya Uturuki ya kulibadili jengo hilo kuwa uchokozi na fedheha kwa ustaarabu katika karne hii ya 21.

Lawama za Ugiriki kuhusu kugeuzwa kwa jengo la Hagia Sophia na kuwa msikiti baada ya jengo hilo kutumika kwa miongo kadhaa kama makavazi, zimezusha mvutano kati ya Ugiriki na Uturuki.

Wakati huo huo ndege za Israeli juzi jioni zilishambulia vituo vya kijeshi vya Syria katika eneo la Quneitra Kusini Magharibi mwa Syria na kuwajeruhi wanajeshi wawili.

Kituo cha televisheni cha serikali ya Syria kimenukuu taarifa kutoka duru za kijeshi kwamba ndege hizo zilishambulia vituo vitatu vya kijeshi muda mfupi kabla ya saa sita usiku.

Shirika hilo pia limeripoti kuwa mashambulio hayo yalisababisha moto katika maeneo kadhaa. 

Katika ujumbe kupitia ukurasa wa twitter, jeshi la Israeli ambalo mara nyingi halizungumzii kuhusu mashambulizi ndani ya Syria, limesema, mizinga ilirushwa kutoka Syria kuelekea Israeli na hivyo jeshi lake likajibu kwa kuvishambulia vituo vya kijeshi vya Syria katika eneo hilo la Kusini na kwamba linailaumu serikali ya Syria.

 Israel imesema litachukuwa hatua wakati wowote inapohisi uhuru wake umekiukwa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,727FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles