21.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Uturuki, Urusi zatathmini vikosi vya mpakani Syria

MOSCOW, URUSI

MAAFISA wa Uturuki na Urusi wanapitia upya usambazaji wa vikosi vyake katika eneo la mpaka wa Syria, Tel Rifaat.

Makamu wa Rais wa Uturuki, Fuat Oktay, ametoa taarifa hiyo hii jana ikiwa ni siku moja baada ya majibizano ya risasi katika eneo hilo kumuua askari wa Uturuki.

Askari wengine wa Uturuki waliuawa na wengine wawili kujeruhiwa katika mashambulizi mawili tofauti yaliyofanywa na wanamgambo wa Kikurdi juzi Jumamosi.

Wizara ya Ulinzi ya Uturuki imesema jeshi la nchi hiyo lilifanya mashambulizi kujibu hatua ya wanamgambo.

Kwa mujibu wa makamu wa rais, jeshi la Uturuki litaendelea na operesheni katika mpaka wake hadi vitisho vyote vitakapoondolewa, akiongeza kuwa ikiwa mashambulizi yataendelea inawezekana kukawepo hatua mpya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,717FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles