24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

UTUMISHI WAANZA SAFARI KUHAMIA DODOMA

Na Daudi Manongi-MAELEZO


Angellah KairukiWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amezindua rasmi safari ya awamu ya kwanza kwa kuaga msafara wa magari yaliyobeba vifaa vya Ofisi vya kundi la kwanza la watumishi 87 wa ofisi hiyo kuelekea mkoani Dodoma.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo, alisema umefika wakati wafanyakazi wa Serikali kuanza safari ya kuhamia makao makuu Dodoma ili kutimiza ahadi iliyotolewa na Rais Dk. John PMagufuli wakati wa Maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa mapema mwaka jana.

“Kufuatia agizo la Rais, Waziri Mkuu kama kiongozi na mratibu wa shughuli za Serikali alihamia Dodoma Septemba mwaka jana, Wizara nyingine zimeendelea na maandalizi ya kutekeleza azma hii ya serikali.

“Nami leo (jana) napenda kutumia fursa hii kuuarifu umma wa Watanzania kuwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekamilisha maandalizi ya kuhamia Dodoma na hivi punde vifaa vya kundi la kwanza vitaondoka kwenda Dodoma,” alisema

Alisema katika kundi la kwanza jumla ya watumishi 87 watahamia Dodoma litahusisha uongozi wa juu wa Wizara ukiwajumuisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu na baadhi ya wakurugenzi, wakurugenzi wasaidizi, maofisa waandamizi na watumishi wengine.

Katika hatua nyingine Kairuki alisema wale wote wanaohitaji kukutana na Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wake wafike katika Ofisi zilizopo Dodoma na kwa masuala yote yanayohusuu Sera na Sheria za Utumishi wa Umma na Utawala wa Utumishi wa Umma kwa ujumla yatatekelezwa mjini humo.

“Masuala ya mishahara, uendelezaji rasilimali watu, ukuzaji maadili, anuai za jamii, uchambuzi ushauri na utendaji kazi na huduma ya teknolojia ya habari na mawasiliano yataendelea kushughulikiwa na ofisi ya Dar es Salaam,” alisema .

Alisema Ofisi yake itafunguliwa rasmi mjini Dodoma Januari 30, mwaka huu ambayo itakuwa katika Jengo la College of Humanities and Social Sciences katika eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma kama makao yake ya muda mpaka hapo itakavyoelezwa vinginevyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles