TOKYO, Japan
MAMIA ya wanafunzi nchini Japan, wameanza kukataa kwenda shule, mtindo ambao unafahamika kama “futoko”.
Mtoto mwenye miaka 10, Yuta Ito alikuwa anasubiri likizo yake kwa hamu ili aweze kuwaambia wazazi wake jinsi wanavyojisikia kuwa hajisikii tena kwenda shule.
Kwa miezi kadhaa amekuwa akihudhuria shule ya msingi kwa kulazimishwa sana, mara nyingi huwa anakataa kabisa.
Alisema alikuwa ananyanyaswa na alikuwa anagombana na wanafunzi wenzie darasani.
Wazazi wake, wakati huo walikuwa na mambo matatu ya kuchagua: Kumfanya Yuta aweze kuhudhuria shule kwa kumueleza umuhimu na vitu ambavyo angeweza kuvipata kama akiweza kwenda shule kwa matumaini kuwa hali itabadilika.
Miongoni mwa mambo waliyokuwa wakimueleza, ni pamoja na kumfundisha nyumbani na kumpeleka shule bila gharama au kubaki nyumbani, naye akachagua namba tatu.
Taarifa zinasema, sasa Yuta anatumia muda wake ambao alipaswa kwenda shule kufanya kile anachojisikia kufanya na ana furaha zaidi.
Yuta ni miongoni mwa wanafunzi wanaotumia mtindo wa futoko, inayomaanisha kwa wizara ya elimu Japan kuwa ni wanafunzi ambao wanaacha kwenda shule kwa zaidi ya siku 30, kwa sababu ambazo hazina uhusiano na matatizo ya masuala ya kiafya au kifedha.
Kutohudhuria huko kwa wanafunzi shuleni huwa kunatajwa kuwa ni utoro, uoga wa shule au mtoto kugoma tu kusoma.
Mpaka mwaka 1992, watoto walianza kukataa kuhudhuria shule na wengi wakadhani ni ugonjwa wa akili.
Lakini mwaka 1997, jina liliadilika na kuwa watoto wasiohudhuria shuleni.
Oktoba 17, Serikali ilitangaza idadi ya wanafunzi watoro shuleni imeongezeka kwa kiwango cha juu, kati ya wanafunzi 164,528 watoto 30 hawahudhurii shule kwa muda wa siku 30 au wanafunzi zaidi walitega shule mwaka 2018, huku mwaka 2017 watoto 144,031 walitega.
Mvutano wa kuwa na shule za bure ulianza Japan mwaka 1980 na kufanya idadi ya utoro shuleni kukua zaidi.
Kuna shule nyingine ambazo zinawapa uhuru wa kujiamulia.
Huwa wanakubali mtu kuchagua masomo ya ulazima pamoja na kujifunza ukiwa nyumbani ingawa hawawezi kutambua masomo hayo ambayo wanapata nyumbani.
Idadi ya wanafunzi wanaohudhuria shule ya bure au shule inayompa mwanafunzi uhuru wa kuchagua masomo badala ya kufuata mfumo wa kawaida zimefungwa miaka kadhaa iliyopita kuanzia ilipoanza kuwa 7,424 mwaka 1992 mpaka 20,346 mwaka 2017 .