28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Utata shambulio lililoua 11 baa za shisha Ujerumani

HANAU, UJERUMANI

KUNDI la siasa za mrengo wa kulia linatajwa kuwa nyuma ya mashambulio mawili yaliyotelezwa jana katika baa mbili za shisha huko magharibi mwa Ujerumani  na kuua watu 11

Tayari waendesha mashataka wanashughulikia shambulio hilo lililotekelezwa katika jiji la Hanau  sawa na na ugaidi, huku mamlaka zikieleza kuwa dalili zinaonyesha kuwa liliwalenga wale wasio wageni.

Inaripotiwa kuwa washambuliaji walifyatua risasi katika baa ya kwanza katikakati mwa mji wa Hanau na kuwaua watu watatu, na kisha baadae walielekea mji jirani wa Kessel na kufyatua risasi tena katika baa nyingine ambapo watu watano waliuawa. 

Baa zilizolengwa na washambuliaji ni zile ambazo watu huzitumia kuvuta shisha katikati mwa mji wa Hanau na katika mji wa Kesselstadt.

Polisi nchini Ujerumani imesema mmoja wa watuhumiwa wa mauaji hayo alikutwa amekufa nyumbani kwake mapema  jana. 

Polisi wa eneo hilo wamesema timu maalumu ya wataalamu ilikuta pia mwili wa mtu mwingine katika nyumba ya mtuhumiwa, lakini hakuna dalili ya mtu huyo kuhusika kwenye mauaji hayo. 

Miili hiyo ni ya mshukiwa wa shambulizi hilo pamoja na mama yake mwenye umri wa miaka 72.

Awali mtuhumiwa wa shambulio hilo anayehusishwa na siasa kali za mrengo wa kulia alituma video kwa njia ya  mtandao yenye urefu wa karibu saa moja akidai kuwa Ujerumani inaongozwa na taasisi ya siri yenye mamlaka makubwa. 

Katika video hiyo alitoa pia kauli dhidi ya wahamiaji kutoka nchi za Kiarabu na Uturuki.

Miili ya watu waliouawa ilikutwa saa kadhaa baada ya milio ya risasi kusikika  saa nne usiku. 

Taarifa ya msemaji wa ofisi ya mwendesha mashitaka wa eneo hilo inasema habari juu ya kuwepo kwa shambulio jingine la risasi katika mji jirani wa Lamboy hazijathibitishwa ingawa kulikuwa na ulinzi  mkali katika eneo hilo. 

Ulinzi zaidi umeimarishwa katikati mwa mji wa Hanau wenye takribani wakaazi 20, 000.

Baada ya shambulio hilo msemaji wa serikali ya Ujerumani ameandika kupitia ukurasa wake wa tweeter kulaani tukio hilo na kutoa pole kwa wakazi wa eneo hilo. 

Naye Meya wa mji huo Claus Kaminsky amesema  tukio hilo ambalo limejeruhi watu wengine watano ni  baya na litasalia vichwani mwa wakaazi wa eneo hilo kwa muda mrefu.

Mamlaka zimeendelea kuwasaka washambuliaji ambao walitoweka eneo la tukio na wanaendelea kuchunguza chanzo cha tukio hilo ingawa ripoti za awali zinaeleza kuwa shambulio hilo lilichochewa na itikadi kali. 

Shirika la habari la Ujerumani dpa limeripoti kuwa polisi wanachunguza video ambayo mshukiwa huyo huenda aliiweka kwenye mtandao wa intaneti akielezea nadharia ya njama kuhusu unyanyasaji wa watoto nchini Marekani. Uhalisia wa video hiyo haujathibitishwa haraka. 

Hanau ni mji ulio katika jimbo la Hesse kilomita chache kutoka Frankfurt.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles