30.4 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

Utata kifo cha profesa wa kichina aliyeuawa Marekani akitafiti corona

 PENNSYLVANIA, MAREKANI

MAUAJI ya raia wa China, mtafiti wa masuala ya virusi vya corona kwenye ardhi ya Marekani, yamesababisha nadharia mbalimbali duaniani kuwa kuna sababu iliyojificha kuhusu kifo chake. 

Bing Liu, profesa msaidizi mwenye miaka 37 katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Pittsburgh, Marekani alikutwa amefariki dunia nyumbani kwake Jumamosi iliyopita.

Wenzake walisema alikuwa karibu kupata “matokeo muhimu” ya tafiti kuhusu Covid-19, tukio lililosababisha kuwepo kwa maoni mitandaoni yanayoeleza kuwa yawezekana Liu aliuawa lakini polisi walisema ni tukio la kujiua. 

Kwa nini Liu aliuawa?

Kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo, mtafiti huyo alikutwa katika makazi yake eneo la Pittsburgh akiwa na majeraha mengi ya risasi kichwani, shingoni 

Mtu aliyekuwa na silaha alitambulika kuwa na miaka 46, mhandisi wa programu ya kompyuta, Hao Gu. Mamlaka zinasema muuaji naye alijiua baada ya kurudi kwenye gari lake.

Liu na Gu walikuwa wanafahamiana, maofisa wapelelezi wa mauaji walieleza.

Uchunguzi umebaini kuwa lilikuwa tukio la kuua na kujiua lililotokana na mgogoro wa muda mrefu wa masuala ya kimapenzi.

‘’Hakuna ushahidi wa kuhusisha tukio hilo na utafiti wa Liu na mazingira ya sasa ya changamoto za kiafya,”walisema wapelelezi hao.

 Liu ni nani? 

Katika taarifa yao wenzake wamemwelezea kama mtafiti wa kipekee ambaye alikuwa ukingoni kufanikisha kupata matokeo muhimu ya kuelewa maambukizi ya Covid-19. 

Waliomboleza kifo cha Liu na kuahidi kumalizia utafiti wake zikiwa ni juhudi za kuenzi ubora wake katika uwanja wa kisanyansi.

Liu, ambaye ni raia wa China alipata shahada yake ya kwanza na shahada ya uzamivu katika masomo ya sayansi ya kompyuta nchini Singapore kabla ya kufanya utafiti nchini Marekani. Aliwahi kuungana na wanabaiolojia wengine kufanya utafiti kuhusu kinga ya binaadamu, kwa mujibu wa wasifu wake mtandaoni. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,873FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles