UTATA KIFO CHA MTOTO ANAYEDAIWA KUBAKWA, KUNYONGWA NA MJOMBA

0
807

 

Mtoto Norah Jimmy (11), enzi za uhai wake

UTATA umeibuka kuhusiana na kifo cha mtoto Norah Jimmy (11), anayedaiwa kubakwa na kisha kunyongwa na mjomba wake, John Msigalla (21), Sinza jijini Dar es Salaam.

Utata huo umeibuka baada ya baadhi ya watu kutofautiana kuhusu chanzo cha kifo cha mtoto anayesoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Atlas ambapo wengine wanadai alijinyonga mwenyewe huku wengine wakidai amenyongwa na mjomba wake ili kupoteza ushahidi.

Tukio la ‘kuuawa’ kwa mtoto huyo limetokea juzi baada ya mtoto huyo kukutwa akiwa ananing’inia kwenye kitanzi kinachodaiwa kufungwa kwenye banda lililopo nje ya nyumba yao kwa ajili ya kumnyonga paka anayedaiwa kuwasumbua.

Mama wa marehemu, Agnes Msigalla ambaye amesema alipata taarifa akiwa njiani kurejea nyumbani kutoka kazini ambapo alitumiwa ujumbe ukimtaarifu kuwa mwanawe ameanguka chooni na amepelekwa Hospitali ya Sinza Palestina.

“Nilikuta tayari ameshafariki lakini wakamfunua na wakanionyesha kwamba alikuwa amebakwa sikutaka kuangalia sana huko maana mtoto wangu ndiyo alikuwa amevunja ungo kama mwezi mmoja tu uliopita, aliyefanya tukio hadi sasa sijajua kama ni watu au ni mdogo wangu maana sikuwepo.

Baba wa marehemu Jimmy Marealle, amesema: “taarifa nimezipata kwa kupigiwa simu na mama yake Norah… nimesikitika sana kwa sababu Norah ni binti yangu pekee, naomba sheria ichukue mkondo wake haki itendeke.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here