25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Utata alipo Askofu Gwajima

gwajimaaNa Veronica Romwald, Dar es Salaam

UTATA umegubika juu ya wapi alipo Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Tanzania, Josephat Gwajima ambaye anasakwa na polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Wakati baadhi ya vyombo vya habari vikieleza kuwa amekimbilia nchini Canada na vingine vikiripoti kuwa  yupo Dubai, Msemaji wa Kanisa hilo, Yekonia Bihagaze amesisitiza kuwa askofu huyo bado yupo nchini.

Akizungumza na MTANZANIA jana baada ya kumalizika kwa ibada ya jumapili katika Makao Makuu ya kanisa hilo, Ubungo jijini Dar es Salaam,  Bihagaze alisema Askofu Gwajima yupo mikoani akiendelea kutoa huduma ya kiroho.

“Si kweli kwamba Askofu yupo nje ya nchi… hao wanaosema hivyo sijui wamezitoa wapi taarifa hizo kwa sababu hata simu zake hazipo hewani, tunachojua sisi viongozi aliotuacha hapa Makao Makuu ni kwamba yupo mikoani akiendelea kutoa huduma za kiroho, alipoondoka alituaga akisema anakwenda huko kwa ajili ya kupeleka neno la Mungu,” alisema.

kutokana na hali hiyo, MTANZANIA, alipoulizwa ni wapi alipo na mkoa gani, Bihagaze, alisema kiongozi wao anaendelea na shughuli za kiroho kama kawaida huku walitaka Jeshi la Polisi kufuata utaratibu na waeleze ni suala gani wanalomtafutia kiongozi wao.

“Hatuwezi kumficha, na wala hatushangai wapi alipo kwa sasa, ni jambo la kawaida katika utendaji kazi wake, huwa anaweza akasafiri akakaa hata miezi miwili au mitatu na hatuna mashaka wala hatuwezi kuuliza maana huwa anafanya vile anavyopewa maelekezo na Mungu,” alisema.

Katika hatua nyingine, Bihagaze alisema anashangazwa na hatua ya polisi kumtafuta askofu huyo huku likiwa halijatoa maelezo kwa maandishi.

“Jeshi lina utaratibu maalumu, linapomuhitaji mtu kwa mahojiano huwa linaandika barua kumuita kwa ajili ya mahojiano hayo, lakini tunasikia tu kwamba linamtafuta.

“Ndio maana hadi leo bado tunaamini kuwa wale waliokwenda kule nyumbani kwa Askofu hawakuwa askari kwa sababu,  hawakuwa na sare rasmi za askari, walikuwa wamevaa kiraia isitoshe hawakuwa na gari la polisi bali la binafsi.

“Sasa tutaamini vipi hapo izingatiwa wapo na majambazi lakini kama Jeshi hilo lingeandika barua ya wito, angerudi, tungemweleza na angekwenda mwenyewe kuhojiwa mbona walifanya hivyo wakati ule wa sakata la Pengo na walimpata,” alisema.

MTANZANIA ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, ili kujua hatima ya kusakwa kwa Askofu Gwajima kwa siku ya nne mfululizo, alisema leo atataoa taarifa yake kwa umma.

“Kesho (leo) nitalitolea ufafanuzi rasmi suala hilo ni vyema usikose,” alisema Sirro.

Juzi, Kamanda Sirro alisema Jeshi hilo linamtafuta Askofu Gwajima kumhoji juu ya mahubiri yake aliyoyatoa Juni 11, mwaka huu kanisani kwake Ubungo jijini Dar es Salaam.

Katika mahubiri hayo yaliyosambaa kwa kasi katika  mitandao mbalimbali ya kijamii, Askofu huyo anasikikika akiukosoa utendaji kazi wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles