30.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Utapenda Shilole, Rostam wanavyocheza na mashabiki

SWAGGAZ RIPOTA

MUZIKI umekuwa mgumu kiasi kwamba msanii asipokuwa na ubunifu hauna shabiki atakayeshughulika naye, ndiyo maana hivi karibuni tumesikia ngoma kali zenye tungo zilizojaa ubunifu ndani yake.

Mfano ni ngoma mpya ya ROSTAM, umoja unaoundwa na wasanii Roma Mkatoliki na Stamina inayoitwa Kijiwe Nongwa ambayo humo ndani mastaa kibao wamechanwa kwa mafumbo yaliyotengenezwa kiufundi na kufanya wimbo huo uwe miongoni mwa nyimbo pendwa kipindi hiki.

Ukisikiliza kwa makini na ukafumbua mafumbo hayo utabaini mastaa kama Diamond Platnumz, Shilole, Wema Sepetu, Hamisa, Irene Uwoya, Dogo Janja, Pierre Liquid, marehemu Ruge Mutahaba, Dudu Baya, Nabii Tito, Dk Shika, Amber Rutty na wengi wengine kutoka tasnia ya siasa wamechanwa.

Miongoni mwa wang’amuzi wa mafumbo hayo ni staa wa muziki na mjasiliamali, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ambaye amebaini kuwa ROSTAM wamemchana yeye na mumewe Uchebe Ashraf ambaye ni fundi magari.

Katika wimbo wa  ROSTAM, kuna mistari Stamina anasema: “Vipi dada yetu wa Igunga, simwoni tena udangani.”

Roma anajibu kwamba: “Mbona ameshapata mchumba siyo vibenteni vya zamani, yule fundi gereji chawa si kamteka bibie na wamefungua mgahawa yaani wote mama ntilie.’.

Sasa inajulikana kwamba staa aliyetokea Igunga mkoani Tabora ni Shilole ambaye ameolewa fundi magari Uchebe na sasa wanamiliki mgahawa wa Shishi Food  kwahiyo mistari hiyo inamgusa moja kwa moja.

Shilole ambaye hivi karibuni amesikika katika wimbo wa Baddest 47 unaoitwa Nikagongee Remix, hakukaa kimya, akaingia studio kurekodi wimbo Sitaki Mazoea wa kuwaponda Rostam.

Katika ngoma hiyo ametumia lugha kali za kashfa na akaiweka katika ukurasa wake wa Instagram ikiwa pamoja na video inayowaonyesha Roma na Stamina wakila ukoko katika mgahawa wake.

Shilole, akaongeza kuwa ataendelea kuwakomesha Rostam zaidia baada ya kuwaondoa kwenye nafasi ya kwanza ya video zinazotazamwa zaidi YouTube kupitia wimbo Nikagongee Remix.

Akizungumza n Swaggaz jana, Stamina alisema: “Shilole ni dada yetu yaani ni dada yetu kipenzi kabisa na sisi ni watani, huwa tunataniana na tulijua tu lazima utumaindi na tunaheshimiana na mumewe Uchebe, hatuna ugomvi tunaheshimu sana ile familia.”

Katika kuonyesha kuwa video aliyoitoa Shilole ikiwaonyesha ROSTAM wakila ukoko ni fursa, wasanii hao wakaanzisha shindano la mashabiki kujirekodi video wakila ukoko huku wakisikiliza wimbo Kijiwe Nongwa, jambo lililoongeza zaidi ukubwa wa wimbo huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles