27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

UTAJIRI WA MADINI TULIOUPOTEZA KWA MIKATABA NA SHERIA MBOVU!

THAMANI ya madini ya dhahabu leo hii katika soko la dunia ni dola za Kimarekani 41,493.72 ambazo ni sawa na Sh milioni 92,833,899.76. 


Wingi wa hazina ya dhahabu hupimwa kwa kizio cha ounces inayoweza pia kusomeka OZ yaani (ozi). Hazina ya Madini ya dhahabu iliyopo Tanzania leo ni  inatajwa kuwa ni ozi milioni 45 ambazo ni sawa na Kilogramu milioni 1,275,872, hii ni kwa sababu kilogramu moja (1) ni sawa na ozi 35.27. 


Kama bei ya kilogramu moja ya dhahabu katika soko la dunia ni dola za Kimarekani 41,493.72 na kwa kuwa hazina (deposits) ya madini ya dhahabu yaliyopo Tanzania ni sawa na Kilogramu milioni 1,275,872 basi thamani halisi ya madini ya dhahabu pekee hapa nchini ni dola za Kimarekani bilioni 52,940,669,123, ambazo ni sawa na Sh Trilioni 118,433,570,897,080. Hakika utajiri huo wa dhahabu pekee unatisha!


Sasa kwa mujibu wa Ripoti ya mwaka 2016 ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), ambayo Rais Magufuli ameivunja bodi yake na kumsimamisha kazi Ofisa Mtendaji Mkuu wa wakala huo; ripoti hiyo ilisema kuwa kwa mwaka 2016 Migodi Mikubwa yote iliilipa Serikali Mrabaha jumla ya Dola za Kimarekani milioni 76.1 (Sawa na Shilingi za Tanzania Bilioni 170.25), Kodi ya Makampuni iliyolipwa ilikiwa Sh bilioni 195, wakati kodi nyinginezo na ushuru ilikuwa ni Sh za bilioni 4.2. 


Ukijumlisha kodi zote zilizolipwa na makampuni ya madini nchini kwa mtiririko huo hapo juu utapata jumla ya kiasi kilicholipwa na makampuni ya madini yote kwa ujumla ni Sh bilioni 369,678,530,000. 
Fedha hizo jumla yake ni sawa na asilimia sifuri ya thamani ya madini ya dhahabu pekee ambayo thamani yake kama nilivyoanisha hapo juu ni Sh trilioni 118.  


Hii maana yake kama kila mwaka makampuni ya madini yakiendelea kulipa kodi zote bilioni 369, basi itachukua jumla ya miaka 696 kuimalizia hazina ya dhahabu iliyo ndani ya ardhi ya Tanzania hivi sasa. 


Na kama makampuni ya madini yanatulipa asilimia sifuri tu ya hazina ya madini ya dhahabu pekee basi sisi Watanzania tumeliwa, tumenyonywa na kunyanyasika kupitia utajiri wetu wenyewe kutokana na viongozi waliopewa dhamana ya kulinda rasilimali zetu kuziuza kwa hasara ya Taifa kwa mikataba ya uchimbaji wa madini waliyoingia na wawekezaji hao, ambao wao huja nchini na mtaji wao na kuondoka na kila kitu cha utajiri wetu uliopo ardhini. 


Hapa nimefanya ukokotozi wa madini ya dhahabu tu sijaanisha thamani ya madini mengine ambayo yapo nchini kama vile Almasi, Chuma, nickel, Copper, Cobalt, na Silver, tanzanite, ruby, garnet, limestone, soda ash, gypsum, salt, phosphate, gravel, sand, dimension, Urani (uranium ) na makaa ya mawe (coal). 


Endapo bajeti ya Serikali ya Tanzania inayotakiwa kugharamia huduma za jamii, miradi ya kimaendeleo na kuigeuza Tanzania kuwa ya viwanda ni Sh trilioni 31.6 basi thamani ya madini ya dhahabu pekee ingeweza kulipia bajeti nzima mfululizo kwa miaka minne. 
Deni la Taifa ambalo ni trilioni 41 lingeweza kulipwa kwa thamani ya kiasi cha dhahabu iliyopo ardhini na tukabakiwa na trilioni 77.43. Huu ni sehemu tu ya Utajiri wa Dhahabu ambao unatunyima usingizi. Taifa linaendelea kuwa masikini wakati nchi ina rasilimali za Kitajiri kiasi hiki. 


Mwisho nitoe maoni yangu kama Mtanzania kuwa kilichofanywa na Serikali kuzuia Makontena 277 ya mchanga wa madini (Makinikia) ni nukta tu ya utajiri mkubwa uliopaswa kulindwa kwa kuwa Taifa kuamua kuwa na mikataba bora na yenye tija kwa Taifa tangu uchimbaji wa madini ya dhahabu ulipoanza nchini. 


Kuzuia makontena yaliyopo bandarini wakati ardhini bado kuna hazina kubwa bila kupitia upya mikataba baina ya Taifa na wawekezaji, sera na sheria zilizopo ni sawa na kufukuza upepo. 
Tukubali kuwa kama Taifa tulijikwaa mahali, hatujachelewa kujisahihisha! Tumepoteza utu wa Taifa kwa kukumbatia mikataba mibovu na ya kifisadi.  


Kuendelea kupata asilimia sifuri tu ya thamani ya madini ya dhahabu pekee kunatokana na uwepo wa mikataba, sheria na sera zilizopo katika tasnia ya uchimbaji wa madini. 


Leo hii ni aibu sekta ya madini kuchangia asilimia 4 tu ya pato la Taifa. Pia ni aibu kuwa na lengo linalotaka sekta ya madini ichangie asilimia 10 ya pato la Taifa ifikapo mwaka 2025. 


Hilo ni lengo dogo sana. Sekta hii pekee inaweza kugharamia bajeti nzima ya nchi na fedha zikabakia. Lazima tuamue, kama tumeamua tusiguse guse, tuchimbe mpaka ndani kabisa!

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles