32.2 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

Utafiti: Wanawake bado wako nyuma kwenye umiliki wa mashamba

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Utafiti wa Wizara ya Kilimo nchini unaonyesha kuwa asilimia 60 ya wakulima ni Wanaume huku wanawake wakiwa ni asilimia 30 tu.

Hata hivyo akizungumzia matokeo hayo leo Januari 10, 2023, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kuwa waneume wanaongoza kwa kumiliki mashamba lakini wanaofanya shughuli za shamba ni wanawake.

“Katika utafiti swali lilokuwa linaulizwa kwa mkulima ni kwamba je unashamba? Utabaini kuwa katika jamii zetu mwanaume ndiye anahesabika kwamba anamiliki mali, lakini ukweli ni kwamba wanaofanya shughuli za shamba ni wanawake.

“Hii inatupa changamoto kwamba kwenye utafiti ujao tutakuwa na maswali haya yote mawili ili kuweza kutenganisha anayemiliki shamba na anayefanya shughuli za shamba, …ila ukweli ni kwamba wanaofanya shughuli za kilimo ni wanawake,” amesema Waziri Bashe.

Kuhusu umri wa wanaojishughulisha na kilimo, Waziri Bashe amesema ni kundi la miaka 18 hadi 40 ndio wanaojikita kwenye kilimo.

“Utafiti pia umeonyesha kuwa kwenye umri walioko shambani ni miaka 18 hadi 40 ndiyo wanaolima tofauti na inavyoaminika kuwa watu wenye umri mkubwa wakiwamo wazee kuwa ndiyo wanaofanya shughuli hizo,” amesema Waziri Bashe.

Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo hadi kufikia Januari 9, mwaka huu zaidi ya wakulima milioni 2.8 wamesajiliwa na mfumo wa kidigitali huku ikisisitiza kuwa mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa njia ya kidigitali umekuwa na manufaa makubwa.

“Mwaka huu wa kilimo mbolea zote zinazotumika nchini zipo kwenye ruzuku tofauti na miaka ya nyuma ambapo ilikuwa ni baadhi tu, pia ruzuku ya Serikali inayotolewa kwa mfumo wa kidigitali ili kuepusha udanganyifu uliokuwa ukifanyika nyuma na inatolewa pale tu mkulima anapokuwa amenunua mbolea.

“Hii pia inarahisisha usimamizi na kuweza kumuona mkulima pale anapokuwa amenunua mbolea, hivyo Mheshimiwa Waziri ametusaidia sana kwani hii pia inatuwezesha kuwa na kanzi data ya wakulima nchini.

“Hadi Januari 9, 2023 zaidi ya tani za mbolea ya ruzuku 194,000 zimeuzwa kwa wakulima zaidi ya 560 na ukomo wa bei ya mbolea ni Sh 70,000 imeeleza Wizara hiyo huku ikisisitiza kuwa mbolea zote kwa mwaka huu zinaruzuku tofauti na miaka ya nyuma huku bei ya juu ikiwa ni Sh 70,000,” imeeleza taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles