25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Utafiti wa mahindi lishe kufanyika kukabili udumavu

Na ELIUD NGONDO,  MBEYA

TAASISI ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Uyole, imeanza kufanya utafiti wa zao la mahindi yenye virutubisho vya lishe ilikupambana na tatizo la udumavu ambalo limekuwa ni changamoto kwa mikoa mingi.

Mtafiti wa zao la Mahindi, Maharage na Soya katika kituo hicho, Leonard Sabula, jana alisema kutokana na changamoto hiyo wao kama watafiti wameamua kuchukua jukumu hilo la kuiunga Serikali kupambana na suala la udumavu.

Sabula alisema taasisi hiyo imekuwa ikifanya tafiti za mazao mbalimbali kwa ajili ya kuwainua wakulima lakini kwa sasa kutokana na tatizo la udumavu, wameamua kutafiti mbegu ya mahindi itakayokuwa na virutubishwo vya kupambana na udumavu.

“Kutokana na tatizo la udumavu hasa kwa mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini, tumeamua kutafiti mbegu mpya itakayo kuwa na virutubishwo kwa ajili ya kupunguza changamoto hiyo,” alisema Sabula.

Alisema kwa uwepo wa mahindi hayo yenye virutubisho tatizo la watoto kutokuwa na akili darasani litakuwa limekwisha kwani miili yao na akili zitakuwa zimeimalika zaidi.

Aidha baadhi ya wakulima wameeleza namna mbegu hiyo ya mahindi ya lishe itakavyo wanufaisha katika kuepukana na tatizo la udumavu wakati vyakula vipo.

Mkulima wa zao la Mahindi Matrida Mwambola alisema wananchi wamekuwa wakilima mazao mengi na kuyatumia kwa chakula lakini suala la udumavu limekuwa ni tatizo kwao.

Alisema kitendo cha watafiti wa taasisi hiyo kutafiti mbegu hiyo ya mahindi itakuwa imesaidia kwa kiwango kikubwa kwani watanzania watakapo kula ugali wa mahindi hayo watapata na virutubishwo vilivyomo ndani yake.

Alisema uwepo wa mbegu hiyo ambayo inavirutubishwa itakuwa ni fursa kubwa kwa wakulima wa zao hilo la mahindi kwani wanaweza kulima na kujipatia kipato kutokana na uhitaji mkubwa utakao kuwepo.

Mkulima mwingine Ponsiana Kibassa, alisema kutokana na kutafitiwa mbegu hiyo ya lishe tatizo la wakulima kukosa soko la mahindi litakuwa limeisha kwa kuwa watumiaji wengi watakuwa ni watanzania wenyewe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles