26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

UTAFITI TWAWEZA WAJA NA MAPYA

Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze

Na FARAJA MASINDE-DAR ES SALAAM

UTAFITI mpya wa 36 uliotolewa na Taasisi ya Utafiti ya Twaweza Dar es Salaam jana, umewachambua Rais Dk. John Magufuli na vyama vya CCM na Chadema.

Kwa mujibu wa utafiti huo uliotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze, idadi ya wanaomuunga mkono Rais Magufuli imeshuka kutoka asilimia 96 mwaka jana hadi asilimia 71, mwaka huu.

Pia, utafiti huo umeonyesha kuwa CCM inakubalika zaidi kwa wazee na watu wasiokuwa na elimu, huku Chadema ikiungwa mkono na wasomi, vijana, wanaume, matajiri na wenye elimu ya kutosha.

Kwa mujibu wa Eyakuze, utafiti huo uligusa mambo tisa na kupewa jina la ‘Matarajio na matokeo, vipaumbele, utendaji na siasa nchini Tanzania’.

“Tumeshuhudia pia uwepo wa kundi ambalo halikukubali wala kukataa utendaji wa Rais ambao ni asilimia 29 kutoka asilimia nne za mwaka jana, huku asilimia tisa wakisema hawamkubali.

“Takwimu zinaonyesha kwamba pengo kubwa la kukubalika kwa Rais Magufuli linaonekana katika makundi ya rika mbalimbali, kwani asilimia 68 ni wenye umri chini ya miaka 30 ikilinganishwa na asilimia 82 ya wenye umri zaidi ya miaka 50,” alisema Eyakuze.

Eneo jingine lililoguswa na utafiti huo ni vyama vya siasa ambalo asilimia 63 walisema wapo karibu zaidi na CCM, huku Chadema kikiwa na asilimia 17.

“Utafiti unaonyesha kuwa CCM inakubalika zaidi miongoni mwa wazee kwa asilimia 80, ikilinganishwa na asilimia 55 za vijana na kwa upande  wa wanawake inakubalika kwa asilimia 68 ikilinganishwa na wanaume wanaoikubali kwa asilimia 58,” alisema.

Kuhusu Chadema, Eyakuze alisema chama hicho kinakubalika zaidi miongoni mwa wanaume, vijana, matajiri na wenye kiwango kikubwa cha elimu.

“Lakini, pale CCM inapoungwa mkono kwa kiwango kidogo, haimaanishi moja kwa moja kuwa Chadema inaungwa mkono kwa kiwango kikubwa,” alisema.

Naye Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, aliwapongeza Twaweza kwa utafiti huo, huku akiitaka Serikali na wawakilishi wa vyama kutilia mkazo suala la upungufu wa chakula.

“Hongereni Twaweza kwa utafiti huu, lakini si kila kitu kilichoandikwa mle ni sahihi. Lakini kilichomo kinaakisi hali halisi ilivyo sasa,” alisema Dk. Salim.

“Kuhusu suala la upungufu wa chakula, kama linatokana na mambo ya uwezeshaji, basi linatakiwa kupewa umuhimu wa aina yake kwa masilahi ya wananchi,” alisema Dk. Salim.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles