31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Utafiti: Mbwa wanaweza kubaini dalili za kifafa

LONDON, UINGEREZA

WANASAYANSI kutoka nchini Ufaransa wamesema wana ushahidi kuwa mbwa anaweza kuhisi dalili za ugonjwa wa kifafa kupitia kunusa.

Kwa mujibu wa timu ya utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Rennes, kina matumaini makubwa kuwa uvumbuzi wao utawezesha wataalamu kubaini mtu mwenye dalili za ugonjwa wa kifafa.

“Inawezekana kuwa mbwa ana pua za ‘kielektroniki’ zinazoweza kunusa harufu inayotoka kwa mtu mwenye dalili ya ugonjwa wa kifafa. Mbwa awali walionyesha kuwa na uwezo wa kunusa harufu zinazoashiria kuwepo wa dalili ya maradhi kadhaa, ikiwemo saratani, malaria na sukari,” umesema utafiti huo.

Baadhi ya watu wenye kifafa huwategemea wanyama. Mnyama mmoja akiwa kwenye chumba alicholala mtoto, anaweza kuitahadharisha familia kuwepo kwa dalili ya kifafa wakati wa usiku wa manane.

Katika utafiti wa hivi karibuni, ulioandikwa katika jarida la ripoti za kisayansi, mbwa watano walipata mafunzo nchini Marekani kubaini harufu ya jasho la mtu aliye na kifafa.

Watafiti wamesema kuwa hatua ya kwanza ni mbwa wawili kati yao walibaini dalili za kifafa karibu kiasi cha theluthi mbili na wengine watatu walikuwa wamepatia kwa asilimia 100.

Ripoti inasema: “Majibu yako wazi kabisa na ilihusisha kubaini harufu ya mtu mwenye dalili ya kifafa. Lakini haijulikani ni kwa vipi dalili za kifafa zinaonekana katika mabadiliko ya harufu.”

Daktari Amelie Catala wa Chuo Kikuu cha Rennes ameiambia BBC: “Utafiti zaidi unahitajika, lakini inawezekana kuwa mabadiliko mwilini husababisha kutoka kwa homoni zinazosababisha kutoa harufu ya aina ya tofauti, lakini nadharia hii bado iko kwenye majaribio.”

Hata hivyo, utafiti huu unaelezwa kuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa, ambapo ripoti inasema itasaidia kuboresha namna ya kutambua dalili za kifafa mapema zaidi, hali itakayoweza kumsaidia mtu kuomba msaada au kujiondoa kwenye maeneo ya hatari kabla ya kuanguka kifafa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles