30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

UTAFITI: Mbegu za kiume zinazuia mimba kuharibika

HASSAN DAUDI NA MITANDAO

MIMBA kuharibika ni moja kati ya changamoto kubwa kwa wanawake.

Hali hiyo inatajwa kuwa ni pale mtoto mchanga aliyepo tumboni anapofariki ndani ya wiki 23 za mwanzo za ujauzito, dalili kubwa ikiwa ni kutokwa na damu ukeni, ikiambatana na maumivu ya tumbo.

Kuonesha ukubwa wa tatizo, kwa Uingereza pekee, mmoja kati ya wajawazito sita hukumbana na hali hiyo, huku sababu zinazotajwa mara kwa mara ni uvutaji sigara (hata kama ni baba pekee), unywaji pombe kwa kiasi kikubwa na matumizi ya dawa za kulevya.

Hata hivyo, kwa mujibu wa utafiti wa Chuo Kikuu cha Afya cha Leiden nchini Uholanzi, wanawake wanaofanya mapenzi ya mdomo wako salama zaidi linapokuja suala la mimba kuharibika.

Taarifa hiyo ni licha ya tafiti mbalimbali zilizowahi kuonya juu ya tabia hiyo ya mapenzi ya mdomo, zikieleza kuwa ni chanzo cha ugonjwa wa saratani ya koo.

Mtaalamu wa afya wa Taasisi ya Saratani ya Marekani, Otis Brawley, aliwahi kusisitiza: “Ndiyo, unaweza kupata saratani ya koo kwa kufanya mapenzi ya mdomo.”

Hata hivyo, madai hayo mapya yameibuliwa na utafiti uliochapishwa na jarida la masuala ya afya la Journal of Reproductive Immunology na kuripotiwa na gazeti la Daily Mail la Uingereza.

“Utafiti wetu umeonesha uhusiano uliopo kati ya matumizi ya mdomo kufanya ngono na tatizo la mimba kuharibika,” ilisema ripoti ya utafiti huo.

Pia inaeleza kwamba mbegu za mwanamume anazomeza mjamzito humsaidia kuimarisha kinga yake ya mwili, hivyo kuimarika kwa afya ya kiumbe kilichopo tumboni.

“Hiyo ni kutokana na mbegu hizo kuwa na homoni na protini,” ilisema ripoti hiyo.

Watafiti wa Chuo Kikuu cha Leiden walifanya uchunguzi wao kwa wanawake 234 waliojitaja kuwa na utamaduni huo wa kufanya mapenzi ya mdomo.

Kati ya hao, asilimia 73 ambao hawakuwahi kupata tatizo la mimba kuharibika, waliwaelezea watafiti kuwa matumizi ya mdomo wakati wa kufanya ngono ni kwa kiasi kikubwa.

Wakati huo huo, wachache waliobaki  ndio waliobainika kuwa na majanga hayo ya mimba kuharibika na walikiri kuwa hufanya mapenzi ya mdomo kwa nadra.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles