26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Ustawi wa Jamii waeleza migogoro ya ndoa inavyochangia unyanyasaji kwa watoto

Mwandishi Wetu -Dar es Salaam

KUONGEZEKA kwa migogoro ya ndoa nchini, kumetajwa kuchochea ukatili na kusababisha watoto kukosa malezi ya wazazi wote wawili.

Kwa mujibu wa takwimu za Ofisi ya Ustawi wa Jamii, kwa kuanzia Julai, 2018 hadi Marchi mwaka huu, mashauri ya ndoa 16,832 yalipokelewa ukilinganisha na mashauri 13,382 kwa mwaka 2017/18.

Hayo katika kikao katika ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na wahariri wa vyombo vya habari chenye lengo la kujengewa uelewa kuhusu ajenda  ya  kitaifa ya wajibu wa  wazazi na walezi kwenye malezi na matunzo ya familia.

Akizungumza katika kikao hicho Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dk. Naftali Ng’ondi, alisema vyombo vya habari ni wadau muhimu katika kutoa elimu kwa jamii hivyo wana wajibu wa kuhakikisha wanatoe elimu itakayosaidia kujengeka kwa malezi bora kwa familia na watoto.

Dk. Ng’ondi alisema vitendo vya ukatili vimekithiri nchini hivyo ameviomba vyombo vya habari kuendeleza ajenda hiyo ili kusaidiana na Serikali katika kupambana na vitendo hivyo.

Alisema kwa mujibu wa utafiti wa hali ya ukatili dhidi ya watoto uliofanyika na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na UNICEF wa mwaka 2011 , mtoto mmoja wa kike kati ya watatu na mmoja wa kiume kati ya saba walifanyiwa vitendo vya ukatili kabla ya kufikisha miaka 18.

Dk. Ng’ondi alisema asilimia 72 ya wasichana na asilimia 71 ya wavulana walifanyiwa ukatili wa kimwili na vilevile robo ya watoto walifanyiwa ukatili wa kiakili.

Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwajuma Magwiza, alisema wadau wote wana wajibu wa kuhakikisha watoto wanapata malezi na makuzi bora kwa kuhakikisha wanajenga maadili na kiumairisha mila na desturi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles