22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

USIYOYAJUA KUHUSU MAJANI YA MSTAFELI

Na MWANDISHI WETU


KWA kawaida matunda na majani yake huwa na faida nyingi mno katika mwili wa binadamu. Wapo ambao wanaweza wasiamini jambo hili lakini huo ndio ukweli halisi.

Leo nitazungumzia umuhimu au faida 12 za majani ya mti wa mstafeli katika afya.

Faida zake

 • Juisi ya majani ya mstafeli hutibu saratani haraka na kwa ufanisi zaidi.
 • Ina nguvu mara 10,000 zaidi ya tiba ya mionzi katika kuziua seli za saratani
 • Hutibu maumivu ya nyuma ya mgongo/low back pain
 • Ni tiba ya asili ya maumivu ya mishipa. Unachopaswa kufanya ni kusaga majani yake hadi yalainike kabisa kisha paka taratibu eneo la mshipa lililo na maumivu mara mbili kwa siku.
 • Hutibu maumivu ya jongo/gout.
 • Hurekebisha usawa wa kiasi cha damu sukari mwilini.
 • Huongeza kinga ya mwili.
 • Hudhibiti ukuaji wa bakteria, virusi, vijidudu nyemelezi na uvimbe.
 • Huongeza stamina ya mwili na kurahisisha kupona haraka unapokuwa mgonjwa.
 • Hutibu jipu na vivimbe.
 • Hukimbiza chawa.

Utatumiaje majani ya mstafeli kama dawa?

Tengeneza chai kutokana na majani freshi ya mstafeli na unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili kwa mwezi mmoja. Inashauriwa hiyo chai unywe nusu saa kabla ya chakula cha mchana na jioni.

Kama hutaweza kupata majani freshi ya mti wa mstafeli unaweza kutumia majani makavu ya mti huu yaliyo katika mfumo wa unga kwenye maduka ya dawa za asili sehemu nyingi hapa Tanzania.

Kwenye hiyo chai ya majani ya mstafeli ndani yake weka vitu hivi pekee; maji ya chai, majani ya mstafeli na asali au sukari, usiongeze majani mengine ya chai humo. Pia inashauriwa utengeneze chai ya kutosha kuitumia kutwa nzima yaani uchemshe vikombe vitatu kwa wakati mmoja na uinywe kikombe kimoja kutwa mara tatu.

Mara nyingi majani ya mstafeli ni vigumu kupatikana lakini kama unauhitaji uweza kuyapata katika maduka yoyote ya dawa asili. Pia unaweza kununua yale yaliyosagwa kabisa ili kuepuka usumbufu.

Makala hii imeandaliwa na Fadhili Paulo ambaye ni tabibu wa dawa asili. Kwa ushauri zaidi WhatsApp +255769142586.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,205FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles