24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

USIMAMIZI SKIMU ZA UMWAGILIAJI KUJENGA TANZANIA YA VIWANDA

Na MWANDISHI WETU – SIMIYU


UANZISHAJI wa vyama vya umwagiliaji kwa ajili ya usimamizi wa skimu za umwagiliaji ni suluhisho la utunzaji wa skimu hizo itakayosaidia Tanzania kuwa ya viwanda kupitia kilimo cha umwagiliaji.

Hayo yalielezwa jana mjini Bariadi katika Viwanja vya Nanenane vya Nyakabindi na Ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Zukheri Huddi, alipokuwa akizungumza na wakulima na waandishi wa habari waliotembelea banda la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Zukheri alisema Sheria ya Umwagiliaji namba 5 ya mwaka 2013 na kanuni zake za mwaka 2015 inahamasisha skimu za umwagiliaji kusimamiwa na kuendelezwa na vyama vya umwagiliaji, ili ziweze kuwa na ufanisi.

Pia alieleza kuwa, ili kilimo cha umwagiliaji kiwe endelevu na chenye tija kuweza kufikia Tanzania ya Viwanda na Biashara, wakulima wote nchini wanaomiliki mashamba katika skimu za umwagiliaji wanatakiwa kujiunga katika vyama vya umwagiliaji, jambo litakalosaidia wakulima kusimamia na kuihudumia miundombinu ya umwagiliaji ili iwe endelevu kwa kulipia ada za uendeshaji, matunzo na matumizi ya maji.

“Kuanzia tarehe ya kuanzishwa kwa chama cha umwagiliaji, katika skimu husika chama hicho kinatakiwa kusajiliwa chini ya sheria na kanuni za umwagiliaji na wakulima wote watatakiwa kuwa wanachama wa chama cha umwagiiaji na watalazimika kutekeleza masharti ya chama hicho,” alisisitiza.

Zukheri alisema chini ya Sheria ya Umwagiliaji na kanuni zake, imeweka bayana kwamba, chama, taasisi au chombo chochote kinachojishughulisha na shughuli za umwagiliaji kitatakiwa kutuma maombi yao kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, kwa kujaza fomu ya maombi ya ukubalifu kisha kitapatiwa cheti cha kukubaliwa.

Maadhimisho ya Siku ya Wakulima nchini, Nanenane, yanaendela katika viwanja vya Nyakabindi, mkoani Simiyu, katika Mji mdogo wa Bariadi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles