25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

USILOLIJUA KUHUSU WANYAMA: SIFA 22 ZA MAMBA, JINSI YA KUMKABILI

WIKI iliyopita tulizungunzumzia sifa za mamba na jinsi anavyoishi, makala ile hatukuweza kuimaliza kutokana na ufinyu wa nafasi. Wiki hii tunamalizi sifa za mamba na jinsi unavyoweza kumuepuka pindi unapokutana naye.

Juma lililopita tuliona sifa nane, leo tutaangalia kunzia sifa ya tisa hadi 22.

 

9. Wakati mwingine huigiza amekufa ili kuwakamata samaki wakubwa kwa urahisi, akiwa majini utaona anazunguka kama anapelekwa na maji, samaki wakubwa hubaki kumshangaa.

10. Kama ilivyo kwa tembo, mamba pia huwindwa na majangiri kinachomponza ni ngozi yake.

11. Aonapo hatari hukimbilia majini na akifika tu hugeuza kichwa chake alikotoka.

12. Mkia wake pia huutumia kama silaha, kumsukumia kiumbe anayejaribu kumshangaa nchi kavu, na ukishaingia kwenye maji naye huja.

 

13. Ni mnyama mwenye sumu kali ya nyongo, na nyongo yake ina sifa hizo kwa kuwa humsaidia katika mmeng'enyo wa chakula, kwani anapokula humeza hata mifupa.

 

14. Ni mnyama anayeua haraka, tofauti na wanyama wengine walao nyama, hivyo kifo chake si cha mateso kama ilivyo kwa simba au chui, ila kwa mtazamaji atapata hofu mara dufu kuliko akiona mauaji ya wanyama wengine.

 

15. Anaweza kunyata katika maji na kiumbe aliyepo pembeni asishtuke kabisa, akiwa mwanadamu ndio kabisa atakosa habari.

 

16. Mamba jike hapendi mambo ya mahaba, mara nyingi hutumia muda mwingi kulikimbia dume.

 

17. Madume kwa sababu ya ukubwa wao na uzito, wakati mwingine hutumia ubabe kulipanda jike lake.

18. Dume la mamba lina msaada mdogo kwa jike, msaada huo hutoa pindi linapokuwa na muda wa ziada. 

19. Kutafuta chakula huweza kushirikiana ikiwa ni pamoja na kutengeneza mtego.

20. Mamba ni mnyama anayeweza kukumaki na akakutegea, kwa mfano ukiwa na tabia ya kuoga mtoni au kuchota maji kila ifikapo saa kumi katika eneo fulani, kuna siku anaweza akakutangulia nusu saa kabla na ukifika tu ndio umekwisha.

21. Anapopambana nchi kavu wakati wote hutumia kutishia zaidi kuliko kushambulia, ila wakati akili yake huielekeza kukuzubaisha ili akusukumie majini.

22. Anapong'ata huvunja kutokana na mfumo wa meno yake ulivyo, kwani meno ya juu na ya chini huyakutanisha pamoja.

 

MBINU ZAKE ZA UWINDAJI

Kwa muonekano unaweza kufikiri kuwa mamba ni mnyama mpole, muonekano wake sivyo alivyo hana huruma kabisa, kwa kuwa wanyama wengine maji ni sehemu ya uhai wao basi kwake huo ndio huwa mtego, kama atakuwa nchi kavu na akatangulia kumuona mnyama yoyote akiwa na uelekeo wa kufuata maji, huondoka nchi kavu ili asionwe na hutangilia majini, na mnyama huyo afikapo tu hujikuta katika hatari kwani mawindo yake ni mashambulizi ya kushtukiza tu.  

 

UKIKUTANA NAYE UFANYE NINI?

 

Ushauri wa pekee ni kukimbia tu, kwani hakuna namna yoyote inayoweza kukufanya utoke salama, mnyama huyu ana nguvu kubwa ya mwili na ni kiumbe ambaye huwezi pambana naye hata ukiwa na silaha kwa sababu ya ngozi yake ngumu.

Epuka kukaa sehemu ambazo kuna uwezekano wa uwapo wa kiumbe huyu ni hatari, sehemu hizo ni kama mito iliyopo vijijini au mbugani, kaa mbali kabisa na fukwe za maziwa na wala usidiriki kunawa au kutaka kunywa maji yake pasina ruhusa ya anayewaongoza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles