31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

USIEMPENDA KAJA

6* Yanga yapania kuitandika African sports kuishusha simba kileleni

Habari mbaya kwa simba wasiyempenda kaja. Hii ni kutokana na ukweli kuwa kama yanga wakiiubuka na ushindi kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya African sprts watawashusha kwenye kilele cha msimamo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kukaa kwa masaa 48.

Yanga kwa sasa inashika nafasi ya pili ikiwa na jumla ya pointi 47, iliteremka kwenye nafasi ya kwanza iliyokuwa ikishikilia baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Azam katika mchezo wao wa ligi Jumamosi, Uwanja wa Taifa.

Katika mchezo wa awali, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 wakiwa ugenini katika Uwanja wa Mkwakwani.

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, ameahidi kikosi chake kuingia uwanjani kikiwa na mabadiliko makubwa baada ya kuumizwa na sare katika mchezo wao uliopita, ili kujihakikishia wanaendeleza harakati zao za kutetea ubingwa wao.

“Hatuhitaji kupoteza mchezo huu, hasa ukizingatia tunajiandaa kuelekea kwenye mchezo wetu wa kimataifa, hivyo tunahitaji kupambana kurudi kwenye nafasi ya kwanza katika msimamo,” alisema.

African Sports yenyewe kwa sasa inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi, ikiwa imejikusanyia pointi 17.

Timu hiyo inaivaa Yanga ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bila kufungana na Majimaji ya Songea.

Wakati huo huo, Yanga inatarajia kuondoka nchini Alhamisi, kuelekea Kigali nchini Rwanda kwa ajili ya mchezo wa Klabu Bingwa Barani Afrika dhidi ya APR ya Rwanda, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Amahoro, nchini humo.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Klabu ya Yanga, Jerry Muro, aliliambia MTANZANIA kuwa, baada ya kumaliza mchezo wao huo wa ligi, timu itajiandaa kwa ajili ya safari hiyo ambapo itaondoka kwa ndege.

Yanga imesonga hatua hiyo baada ya kufanikiwa kuitoa timu ya Cercle de Joachim ya Mauritius kwa jumla ya mabao 3-0, ikishinda ugenini 1-0, kabla ya kumalizia kazi Uwanja wa Taifa kwa kuwatandika bao 2-0, mashujaa wakiwa Thabani Kamusoko na Amissi Tambwe.

Hii itakuwa mara ya pili kwa Yanga kukutana na APR katika hatua ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1998 na timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Kigali, nchini Rwanda na kumaliza kwa sare tena ya 1-1 katika mchezo wa marudiano uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles