LONDON, UINGEREZA
UCHAGUZI uliofanyika juzi nchini Uingereza na ambao ulionekana ni vigumu kutabiri matokeo yake, hatimaye chama cha Conservative kimeshinda kwa kupata viti zaidi ya 364 kati ya 650 kuliko ilivyotarajiwa na hivyo kuwaacha wengi katika hali ya mshangao.
Chama hicho ambacho kilitikiswa ndani ya bunge kutokana na hoja ya Brexit kabla ya kuitishwa kwa uchaguzi huo pia kimenyakua ngome muhimu zilizokuwa zikishikiliwa na chama pinzani cha Labour.
Wakati Labour kikionekana kupoteza viti 59 chama cha Conservative kimeongeza viti vipya 47 na Scottish National Party (SNP) kikijinyakulia viti 48 kati ya hivyo 13 vikiwa vipya.
Kiongozi wa chama cha Conservative, Boris Johnson amewashukuru wapiga kura wa Uingereza kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi huo.
Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya chama chake kushinda Jonhson amesema hatua hiyo inaipatia serikali mpya fursa ya kuheshimu maamuzi ya kidemokrasia ya raia wa Uingereza ili kuliimarisha taifa hilo.
Chama cha Johsnon kilihitaji kujipatia viti 326 ili kutangazwa kuwa mshindi lakini kimepitisha idadi hiyo na kufikia viti 364.
Waziri huyo mkuu amesema uamuzi huo unampatia jukumu la kufanikisha Brexit na kuiondoa Uingereza katika muungano wa Ulaya.
”Zaidi ya yote nataka kuwashukuru watu wa taifa hili kwa kujitokeza kupiga kura ya Disemba ambayo imebadilika na kuwa ya kihistoria, ambayo inatupatia sisi kama serikali mpya fursa ya kuheshimu uamuzi wa kidemokarsia wa raia wa kulibadilisha taifa hili na kuonyesha uwezo wa raia wa taifa hili”.
Johnson amesema atafanya kazi ‘usiku na mchana’ ili kuwalipa wapiga kura waliomuonyesha uaminifu baada ya kukisadia chama chake cha Conservative kupata ushindi wa kihistoria.
Huku ikiwa imesalia maeneo mawili ya bunge kutangazwa , chama cha Coservative kina wingi wa viti 76.
Akiungumza mjini London , waziri mkuu Johnson alisema kwamba ni jukumu lake kuindoa Uingereza katika muungano wa EU .
“Raia wanataka mabadiliko” , alisema, ”hatuwezi kuwavunja moyo na hatutawavunja ”
Hatua hiyo inajiri muda mchache baada ya mpinzani mkuu wa Jonson, Jeremy Corbyn kusalimu amri na kusema kwamba hatokiongoza tena chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.
Uamuzi huo wa Corbyn unajiri huku chama hicho kikikabiliwa na matokeo mabaya zaidi ya uchaguzi katika miongo kadhaa.
Fay Jones , Virginia Crosbie na Sarah Atherton atawakilisha chama cha Conservative katika eneo la West Minister
Chama cha Labour kimepoteza viti kaskazini mwa England , Midlands na Wales yakiwa ni maeneo yaliyopiga kura ya Brexit katika kura ya maoni ya 2016.
Labour inatarajiwa kushinda viti 61 ikiwa ni chini ya viti ilivyoshinda 2017 imedaiwa.
Baadhi ya maeneo bunge kama vile Darlington ama Workington , kaskazini mwa England yataongozwa na mbunge wa Chama cha Conservative kwa mara ya kwanza katika miongo kadhaa- ama katika matukio ya Bishop Auckland na Blyth Vally kwa mara ya kwanza tangu viti hivyo kubuniwa.
Lakini Labour kimeshinda kiti cha eneo bunge la Putney, kusini magharibi mwa London kutoka kwa Conservative.
Chama cha Uskochi cha kitaifa kimepata ushindi wake wa kwanza, kikishinda eneo bunge la Rutherglen na Hamilton magharibi kutoka kwa chama cha Labour na Angus kutoka kwa Conservative.
Imebainika kwamba Conservative watapata wabunge 357 ikiwa ni wabunge 39 zaidi ya uchaguzi wa 2017 kura zote zitakapohesabiwa.
Chama cha Labour kitajipatia wabunge 201, SNP wabunge 55 , Liberal Democrats 13, Plaid Cymru 4 The Greens 1 brexit Party 0.
Ongezeko la wastani katika kura ya chama cha Conservative ni asilimia 2 ikiwa ni pointi moja ya kilichotarajiwa katika kura hiyo.
Kura ya chama cha Labour ilipungua kwa asilimia 9 kulingana na utabiri wa matokeo ya kura hiyo yasio rasmi.
Nchini Uskochi, kumekuwa na ongezeko la asilimia 9 katika chama cha kitaifa cha Uskochi – ikiwa ni kiwango cha chini ya ilivyotabiriwa kwa asilimia 13 lakini SNP kinaelekea kushinda viti 55.
Waziri wa masuala ya ndani wa chama cha Conservative, Priti Patel alisema kwamba serikali itahakikisha Brexit inafanyika kwa haraka kabla ya Krisimasi kupitia kuwasilisha miswada iwapo serikali yake itarudi mamlakani.
Mbunge wa zamani wa Conservative, Sir Alan Duncan ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa Boris Johnson amesema kwamba waziri mkuu huyo sasa ndiye mwanasiasa mwenye umaarufu mkubwa Uingereza na kwamba uchaguzi huo umethibitisha hilo.
Mgogoro ulikuwa tayari umezuka katika chama cha Labour kuhusu ni nani anayefaa kulaumiwa kutokana na matokeo mabaya kuwahi kutokea katika miongo kadhaa.
Ilikuwa ni siku mbaya kwa chama cha Labour huko Wales na hususan eneoa la Kaskazni Mashariki.
Mwenyekiti wa Labour, Ian Lavery ambaye alihifadhi kiti chake kwa uchache wa kura alizopata awali amesema kwamba amesikitishwa na wapiga kura katika ngome za chama cha Labour wanaomboleza kuhusu msimamao wa Brexit wa chama hicho.
Kansela kivuli John McDonald aliambia BBC kwamba matokeo ya kura yasio rasmi yalikuwa yanasikitisha kwa Labour.
”Nilidhania ushindani utakuwa wa karibu mno” , alisema na kulaumu kile alichokitaja kuwa uchaguzi wa Brexit.
Baadhi ya wagombea wa Labour wamekosoa uongozi wa Corbyn .
Gareth Snell alisema alitarajia kupoteza kura ya Stoke Central kwa chama cha Conservative na alimtaka Corbyn na McDonald kuondoka lakini pia akawalaumu wanachama wa chama hicho wanaopinga Brexit kwa kukisukuma sana chama hicho.
Ofisi ya waziri mkuu katika taarifa yake imesema kwamba iwapo matokeo hayo yasio rasmi yatathibitishwa na Johnson kurudi uongozini kutakuwa na mabadiliko machache ya baraza la mawaziri siku ya Jumatatu.
Muswada wa makubaliano ya kujiondoa utakaorahisisha kuondoka kwa Uingereza Januari 31 utasomwa kwa mara ya pili katika bunge Disemba 20.
Mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri yatafanyika mwezi Februari, baada ya Uingereza kuondoka EU huku taarifa ya bajeti ikitolewa mwezi Machi.
Huu ni uchaguzi wa Uingereza wa tatu chini ya miaka mitano na wa kwanza kufanyika mwezi Disemba katika kipindi cha miaka 100 na umetawaliwa na kura ya maoni ya 2016 ya kuondoka katika muungano wa Ulaya.
Wakati wa kampeni Johnson aliahidi kuiondoa Uingereza EU kufikia Januri 31, 2020 iwapo angepata wingi wa kura.
Chama cha Labour kilifanya kampeni ya kuongeza matumizi katika huduma za umma mbali na katika vituo vya afya.
Chama cha Liberal Democrats kiliahidi kufutilia mbali Brexit iwapo kiongozi wake Jo Swinson angechaguliwa kuwa waziri mkuu, lakini kura ya maoni ilitabiri kwamba ufuasi wao utapungua wakati wa kampeni.
Chama cha kitaifa cha Uskochi kilisema kwamba uungwaji mkono wao utaashiria kura ya maoni ya pili kufanyika.
Kiongozi wa SNP Nicola Sturgeon alituma ujumbe wa twitter akisema kuwa kile kinachoonekana kuwa ‘kikubwa ni kidogo’.
Caroline Lucas ambaye matokeo hayo yanaonyesha kwamba anatarajiwa kuwa mbunge wa pekee wa chama hicho cha Green Party , alituma ujumbe katika twitter akisema: “Iwapo matokeo haya ni ya kweli basi ni pigo kubwa kwa hali yetu ya hewa kwa kizazi kijacho na demokrasi yetu”.
Kiongozi wa chama cha Liberal Democrat, J Swinson amesema kwamba atajiuzulu baada ya kupoteza kiti chake kwa chama cha SNY kwa kura 149.
Swinson ambaye alianza kampeni akisema huenda akawa waziri mkuu mpya wa Uingereza alijipatia kura 19,523 ikilinganishwa na kura 19,672 za mgombea wa chama cha SNP Amy Callaghan katika eneo la Dunbartonshire mashariki.
Sir Ed Davey na Barones Sal Brinton watakuwa kaimu viongozi wa chama hicho , wakati huu ambapo sio mbunge tena.
Swinson alisema matokeo ya uchaguzi huo yataleta aibu kwa wengi.
Chini ya sheria za chama chama cha Liberal Democrat ni sharti kiwe na kiti kimoja bungeni.