USHER: TANZANIA INANIVUTIA

0
532

NEW YORK, MAREKANI


STAA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Usher Rymond, ameweka wazi hisia zake kwa kusema kwamba amevutiwa na Tanzania.

Msanii huyo alikuwa nchini wiki iliyopita akiwa na familia yake na kutembelea sehemu mbalimbali za kitalii kama vile hifadhi ya Serengeti.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, msanii huyo aliposti picha akiwa na familia hiyo ambayo alipiga kwenye hifadhi hiyo na kuandika: ‘Hii safari imekuwa ya furaha sana, nimejifunza na kuyaona mengi nikiwa na familia yangu, tumevutiwa na mambo mengi sana.’

Safari ya msanii huyo hapa nchini ilikuwa kwa ajili ya mapumziko mafupi, lakini hakutaka ijulikane mapema hadi pale alipoanza kuzisambaza picha zake kwenye mitandao ya kijamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here