33.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

USHABIKI UMEFANYA RIDHIWANI AELEWEKE TOFAUTI

Ridhiwani-Kikwete

NA CHRISTOPHER MSEKENA

WIKI hii kwenye tasnia ya burudani habari kubwa ilikuwa ni ile ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, kumkabidhi bendera ya Taifa, msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Lengo la kumkabidhi bendera hiyo ni kwenda kuitangaza Tanzania kwenye ufunguzi wa michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) nchini Gabon.

Tukio lile lenye mvuto wa aina yake lilifanyika kwenye Ukumbi wa Serena Hotel ambako waandishi wa habari walihudhuria kushuhudia tukio lile ambalo Dstv walihakikisha safari ya Diamond Platnumz inakamilika.

Baada ya taarifa hiyo kuwafikia mashabiki wa muziki na soka Tanzania, mitazamo tofauti ikazaliwa kati yao ambapo wapo walioamini kuwa Diamond alistahili kukabidhiwa bendera hiyo ili kuendelea kuitangaza sanaa ya nchi yetu.

Hali kadhalika kuna kundi la watu wengi waliopinga tukio lile kwa kudai kuwa Diamond Platnumz anakwenda kutumbuiza tu na si kucheza soka hivyo hakustahili kupewa bendera ili akaliwakishe Taifa, ilitakiwa aende kimya kimya kama anavyokwenda kwenye maonyesho yake mengine.

Mzozo ulikuwa mkali mpaka watu mbalimbali maarufu wakawa wanatoa mawazo yao juu ya tukio la Diamond Platnumz kukabidhiwa bendera ya Taifa.

Miongoni mwao ni huyu mdau wa muziki na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ambaye naye alitoa mtazamo wake ambao ulipokelewa tofauti na dhamira aliyoikusudia.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ridhiwani aliandika: “TFF nadhani mnajua kuwa Mungu wa Watanzania anawaona. Tumefika hapa baada ya mpira kutushinda kabisa, sasa tunatoa bendera kwa wanaokwenda kuburudisha na siyo wanamichezo tena…….. Ngashindwa mie”.

Hayo ni maneno mafupi yaliyobeba ujumbe mwanana kwenda kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Dhumuni ambalo naliona mimi hapa, Ridhiwani alitaka wahusika wa masuala ya michezo waone udhaifu wao ambao umefanya badala ya kuipeleka Taifa Stars ikashiriki Afcon anakwenda Diamond Platnumz kutumbuiza.

Maneno hayo ya Ridhiwani yaliibua mjadala mwingine kuwa anapinga kitendo cha Diamond Platnumz kukabidhiwa bendera kwa kuwa yeye ni shabiki wa damu wa Ali Kiba.

Ushabiki usio na maana ulipotosha kabisa nia ya dhati ya Ridhiwani kuikumbusha TFF majukumu yake ya kuhakikisha Tanzania inafanya vyema kwenye medani ya soka.

NUKUU

“Nini kifanyike uzalendo wa nchi tuliousoma kwa wazee wetu uweze kurudi? Tanzania bado tuna deni kubwa la uzalendo,”

Mrisho Mpoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles