22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Usambazaji Maji Dar wafikia asilimia 85

Tunu Nassor – Dar es Salaam  

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo amesema usambazaji wa maji kwa jiji la Dar es Salaam umefikia asilimia 85 huku lengo likiwa ni kufikia asilimia 90 mwishoni mwa mwaka huu.

Akipokea maoni ya wananchi wa Kimara leo Juni 15, mwaka huu Profesa Mkumbo amesema hali ya upatikanaji wa maji kwa sasa imeimarika hivyo Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) inatakiwa kutenga siku ya kupokea maoni ya wateja wao.

“Maji kwa jiji la Dar es Salaam tumefikia asilimia 85 hivyo ni jukumu la mamlaka kutenga siku ya kuwasikiliza wateja ili kujua changamoto na hata pongezi kutokana na huduma wanazotoa,” amesema Kitila.

Amesema kwa sasa maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam yaliyokuwa na tatizo sugu la maji yameanza kupata huduma hiyo.

Naye Meneja wa Mkoa wa Kihuduma wa Dawasa Ubungo, Paschal Fumbuka amesema jumla ya miradi mitatu mikubwa inatarajiwa kuanza Julai Mosi na kukamilika mwezi Septemba.

Amesema miradi hiyo itakwenda kujibu changamoto za maji katika maeneo ya Golani, Saranga na Malambamawili.

“Tuna baadhi ya maeneo ambayo hatujafikisha huduma lakini kabla ya mwaka huu kuisha tutakuwa tumewafikia,” amesema Fumbuka.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kata ya Saranga, Irene Dafa ameishukuru Dawasa kwa kuweza kupeleka maji katika kata hiyo ambayo haikuwahi kuwa na huduma hiyo kwa miaka mingi.

“Dawasa wameweza kuleta maji mitaa nane kati ya tisa tuliyonayo Saranga hivyo tunaomba mtaa uliobaki wa Mkombozi, waumalizie ili tuwazibe midomo wanaofanya siasa kupitia kukosa maji mtaa huo,” amesema.      

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles