30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 9, 2022

USAFI UNAMWONGEZEA MVUTO MTOTO

 

 

NA AZIZA MASOUD,

MTOTO anahitaji kuwa katika mazingira ya usafi wa hali ya juu muda wote ili kumkinga na mambo mbalimbali, ikiwamo maradhi.

Usafi, hasa upande wa mavazi ni njia pekee ya kumuepusha mtoto na baadhi ya maambukizi ya maradhi yatokanayo na uchafu, ikiwamo  ugonjwa wa ngozi na mengineyo.

Aidha, nguo chafu, hasa za ndani kwa watoto, mfano nepi na chupi humfanya mtoto kuchunika mapaja, hali inayosababishwa na kukaa na unyevunyevu kwa muda mrefu.

Mbali na madhara hayo, mtoto msafi huwa na mvuto na kuwafanya baadhi ya watu wapende kumbeba mara kwa mara.

Kuna baadhi ya wazazi ni wavivu kuwaweka watoto wao katika hali ya usafi, hivyo humvalisha  mtoto  nguo moja siku nzima bila kumbadilisha.

Mtoto mdogo anapaswa kubadilishwa nguo hata zaidi ya mara nne kwa siku kulingana na mazingira anayocheza na eneo analoishi.

Muda wa asubuhi mtoto anapaswa kuoga mara mbili pamoja na kubadilishwa nguo, ambapo mara nyingi inakuwa baada ya kuamka na baadaye baada ya kunywa uji au kula chakula,  vivyo hivyo kwa mchana.

Mpe uhuru acheze na wenzake, huku ukimuangalia kama hajajisaidia kwenye nguo, katikati ya saa tano na sita unapaswa kumuingiza ndani, hapa unaweza kumnawisha tu ama kumwogesha na kumbadilisha tena nguo.

Baada ya hapo mwache mtoto achague kama anahitaji kulala au kucheza, lakini ikifika saa nane hakikisha unamwogesha na kumbadilisha tena nguo.

Usafi wa usiku, hasa katika kuoga utategemea na hali ya hewa, ikiwa baridi sana unaweza ukamfuta kwa kitambaa laini, kumbuka kumbadilisha nguo anapojisaidia kipindi chote, huku akiwa anasubiri kulala.

Jinsi ya kufua nguo za mtoto

Mzazi unapaswa kuwa makini katika kufua nguo za mtoto, hakikisha unatenganisha nguo za rangi na nguo nyeupe, hasa nepi.

Mbali na kuangalia rangi, pia unapaswa kuangalia aina ya uchafu, epuka kuchanganya nguo za mtoto aliyejisaidia haja kubwa ama zenye uchafu mwingi na nguo za mikojo.

Gauni za rangi na nguo nyingine zinapaswa zifuliwe tofauti na nyeupe.

Baada ya kufua tafuta dawa za kunyunyizia nguo za watoto ili kuondoa harufu ya shombo ya maziwa.

Hakikisha unaanika kwenye kamba na zinakauka sawasawa na baadaye zinyooshwe pasi ili kuua vijidudu, zikunje vizuri na kuziweka kabatini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,291FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles