31.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

URUSI YAITAKA NATO KUJITOSA VITA DHIDI YA MIHADARATI

MOSCOW, URUSI


SERIKALI ya Urusi imelitaka Jeshi la Jumuiya ya Kujihami ya Magharibi (NATO) kuangalia uwezekano wa kuungana katika vita dhidi ya dawa za kulevya zinazosafirishwa kutoka Afghanistan.

Wito huo umetolewa mjini hapa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergey Lavrov wakati akihutubia mkutano wa kimataifa wa taasisi zinazojihusisha na mapambano dhidi ya dawa hizo haramu.

Katika hotuba hiyo, Lavrov alisema kwa sasa kuna wimbi kubwa la wafanyabiashara wa mihadarati zinazosafirishwa kutoka Afghanistan ambako fedha zinazopatikana pia hutumika kufadhili ugaidi.

“Tunawaomba wawakilishi wa jeshi la NATO kuangalia uwezekano wa kuungana na taasisi hizi ili kukomesha biashara ya usafirishaji dawa za kulevya na magaidi wanaofadhiliwa na wasambazaji kutoka Afghanistan,” alisema.

Lavrov alikumbushia kuwa mafanikio ya ugaidi hutokana pia na fedha kutoka biashara hiyo, jambo ambalo limekuwa likiyafanya makundi hayo kuwa na nguvu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles