28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Urusi yafungiwa kusajili wachezaji wa Uturuki

071214-13-SOCCER-Vitaly-Mutko-OB-PI.vadapt.620.high.94MOSCOW, URUSI

KLABU za nchini Urusi zimefungiwa kufanya usajili kwa wachezaji wa nchini Uturuki kuanzia Januari mwakani kutokana na migogoro ya kisiasa.

Nchi hizi mbili zimekuwa na migogoro ya kisiasa, ambapo wiki iliyopita ndege ya kivita ya nchini Urusi ililipuliwa na jeshi la nchini Uturuki kwenye mpaka wa Syria, Novemba 24 mwaka huu na kuua rubani mmoja huku mwingine akiwa salama.

Waziri wa Michezo nchini Urusi, Vitaly Mutko, aliliambia gazeti la R-Sport new la nchini humo kwamba, hakuna klabu yoyote ambayo itaruhusiwa kusajili wachezaji kutoka nchini Uturuki.

“Kutokana na mgogoro unaoendelea klabu zote za Urusi hazitakiwi kusajili wachezaji ambao wanatoka nchini Uturuki wakati wa usajili wa Januari, lakini kama kuna wachezaji ambao tayari wamesajiliwa wao wataendelea kuzitumikia klabu zao hadi pale mwisho wa mikataba na hawatoruhusiwa kuongeza baada ya kwisha.

“Hata hivyo, kama kuna wachezaji ambao wanaona bora waondoke kwao, wala hakuna tatizo wanaweza kuondoka,” alisema Mutko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles