TEL AVIV,Israel
WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema maofisa wa jeshi la hapa na Urusi watakutana siku chache zijazo mjini Moscow kwa ajili ya kujadili hali ilivyo nchini Syria.
Waziri Mkuu huyo aliyasema hayo jana katika mkutano wake na viongozi wa serikali na akasema kwamba tayari alishazungumza na Rais wa Urusi, Vladimir Putin
“Jana (juzi) nilizungumza na Rais wa Urusi Vladimir Putin. Tulikubalina kwamba wajumbe wetu wa kijeshi ambao wanashirikiana nchini Syria wakutane kwa haraka iwezekavyo na suala hili nadhani litafanyika siku chache zijazo na pia nina matumaini watakutana mjini Moscow,”alisema waziri mkuu huyo.
Idara ya Habari ya Ikulu ya Urusi ilieleza kuwa Rais Putin na Waziri Mkuu Netanyahu walifanya mazungumzo kwa njia ya simu juzi na kisha wakakubaliana kukutana hana kwa hana baadae.
“Kupitia mawasiliano hayo ya simu viongozi tumekubaliana kukutana mjini Paris, ili kuhakikishiana kuzidi kushirikiana kati ya majeshi ya Urusi na Israel tuliouanzisha kwa iaka mingi iliyopita,”alisema Netanyahu .
Viongozi hao pia wamewahi kufanya mazungumzo mjini Paris Novemba 11 mwaka huu wakati wa maadhimisho ya kumbkumbu ya vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.