Ureno yatangaza kupeleka wanajeshi Msumbuji

0
490

-Ureno

Waziri wa mambo ya nje nchini Ureno, Augusto Silva ametangaza rasmi kupeleka wanajeshi katika nchi ya Msumbiji, kufuatia mashambulizi ya kigaidi ya kundi la kiislam mji wa Kaskazini mwa nchi ya msumbiji.

Waziri Silva amesema wanajeshi 60 wanajiandaa kuelekea msumbiji kushirikiana na wanajeshi wa nchi hiyo dhidi ya mashambulizi ya kigaidi.

Mamia ya magaidi wa kundi la kiislam walivamia mji wa palma katika mkoa wa Cabo Delgado na kuwaua raia wa msumbiji.

Pia maelfu ya watu wamekimbia makazi yao wakiwemo raia wa kigeni wanaofanya kazi katika Kampuni ya Kawi inayohusiana na  Mradi wa gesi asilia unaogharimu zaidi ya fedha za kimarekani dola bilioni moja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here