24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Urali wa biashara Tanzania, Misri kuimarika

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Misri kinatarajiwa kuongezeka kutokana na kuwapo kwa jitihada za za kuzalisha zaidi na kutumia fursa ya biashara kati ya nchi hizo.

Akizungumza leo Julai 9,2024 wakati wa kongamano la biashara ikiwa ni siku maalumu ya Misri katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade), Profesa Ulingeta Mbamba, amesema Misri ina fursa nyingi endapo zitatumiwa vizuri.

“Tumesikia fursa zilizopo Misri na namna tunavyoweza kufanya Tanzania kwa ajili ya nchi ya Misri. Bado tunapeleka vitu vya Dola milioni moja lakini sisi tunachukua Dola milioni 60, kwahiyo kama Tanzania tuna vitu vingi vya kujifunza na kuwapelekea wenzetu, tunaweza kufanya biashara ya chakula, vifaa vya umeme na vingine…ni nchi yenye fursa nyingi kama tutaitumia vizuri,” amesema Profesa Mbamba.

Meneja Uenezi na Masoko wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Hamis Dunia, amesema wametumia kongamano hilo kutangaza fursa zilizoko katika Uchumi wa Buluu ambayo ndiyo ajenda ya taifa.

“Uchumi wa Buluu maana yake tunatangaza fursa zilizomo kwenye bahari na pembeni ya bahari, kuna utalii, uvuvi, kilimo cha mwani, usafiri wa bahari, uwepo wa mafuta na gesi kwahiyo tunatafuta wawezekezaji wa kuwekeza. Tunatafuta wawekezaji pia katika ujenzi wa nyumba za biashara na makazi…tuko hapa kutafuta wawekezaji kutoka Misri na sehemu zingine,” amesema Dunia.

Balozi wa Misri nchini, Sherif Abdelhamid, ambaye alifungua kongamano hilo amesema Tanzania na Misri zina historia ya ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji hivyo anaamini kwa jitihada zinazoendelea biashara baina ya mataifa hayo itazidi kukua.

Katika maonesho hayo nchi zinazoshiriki kila moja imetengewa siku maalumu ya kueleza fursa walizonazo na namna wanavyoweza kuimarisha uhusiano wa kibiashara n

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles