31.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

Urafiki, mazoea vyawaponza wachezaji Prisons

abdul-mingange-1Na PENDO FUNDISHA-MBEYA

KOCHA mkuu wa timu ya Tanzania Prisons, Abdul Mingange, amesema urafiki na mazoea yaliyopo kati ya wachezaji wake na timu pinzani yamewaponza na kuwakosesha ushindi dhidi ya Mbeya City.

Timu za Prisons na Mbeya City zilikutana juzi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya na kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Akizungumza na MTANZANIA juzi baada ya mchezo huo, Mingange alisema mchezo ulikabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ya wachezaji kujisahau na kucheza kirafiki zaidi kutokana na ukaribu wa timu zote mbili.

Mingange ambaye msimu uliopita aliifundisa timu ya Ndanda FC ya Mtwara, alisema michuano ya Ligi Kuu Bara msimu huu ni migumu ukilinganisha na msimu uliopita.

“Wachezaji wote walikuwa wakicheza kirafiki zaidi na kusababisha matokeo ya sare ambayo ni tofauti kabisa na yale yaliyokuwa yakitegemewa na makocha, jambo ambalo sikupendezwa nalo,” alisema.

Aidha, kocha huyo alisema wachezaji bado hawajatimiza kile anachotaka kutokana na kuwafundisha kwa muda mfupi tangu akabidhiwe kikosi hicho, huku akieleza kuwa watakapokuwa sawa wataweza kufikia malengo hayo.

“Kwa michezo iliyochezwa msimu huu, timu nyingi zinafanya vizuri zaidi ugenini na kupoteza nyumbani, hivyo nitakachokifanya kwa sasa ni kuandaa mikakati na mbinu za kukabiliana na ushindani viwanjani,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,586FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles