22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Upungufu wa umeme unachangiwa na kukua kwa uchumi-TANESCO

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limebainisha kuwa asilimia 12 ya changamoto ya upungufu wa umeme katika vituo vyao vya uzalishaji unachangiwa na ongezeko la mahitaji ya umeme kutokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi na upungufu wa maji kwenye vituo vya kufufua umeme.

Akizungumza Septemba 27, jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissim Nyamo-Hanga amesema changamoto hiyo inatokana na madiliko ya tabia ya nchi pamoja na matengenezo yanayoendelea baadhi ya visima vya gesi asilia na mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi asilia.

Amesema kutokana na hali hiyo baadhi ya maeneo nchini yamekuwa yakikosa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti upungufu wa megawat 400 kutoka vyanzo vya mabwawa.

“Kutokana na ukame umeathiri mabwawa yetu na matengenezo ya Ubungo namba moja, namba mbili na Kinyerezi tunazalisha megawati 1,900. Tuna upungufu wa megawati 400 na kiwango cha megawati 100 hupungua ndani ya miezi miwili,” amesema Mhandisi Nyamo-Hanga.

Amesema wanaendelea kubuni vyanzo vingine ili kuweza kupata umeme wa kutosha nchini.

“Shirika linaendelea kukamilisha utekelezaji wa mradi wa Bwawa la kufufua umeme la Julias Nyerere litakalokuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 2115 ambao hadi sasa umefikia asilimia 12, “amesema Mhandisi Nyamo-Hanga.

Amesema pindi mradi huo ukikamilika na kuingizwa kwenye gridi ya taifa utachangia kuimarika kwa hali ya umeme chini kwa kiasi kikubwa ndani ya miaka 10.

Aidha, amewaomba wateja kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mpito na Shirika linaendelea kutoa taarifa za upatikanaji wa umeme.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles