23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Upungufu wa madarasa wasababisha wanafunzi 12,000 kutochaguliwa sekondari

Derick Milton, Simiyu

Wanafunzi 12,584 sawa na asilimia 50.4 ya waliofaulu mtihani wa taifa darasa la saba mwaka huu mkoani hapa, wamekosa nafasi ya kuchaguliwa kujiunga elimu ya sekondari kidato cha kwanza mwaka 2019.

Wanafunzi hao ni kati 24,983 waliofahulu mtihani huo mwaka huu, ambapo 12,399 sawa na asilimia 49.6 ndiyo wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2019 katika awamu ya kwanza ya uchaguzi.

Akitangaza matokeo hayo ya wanafunzi waliochaguliwa leo Ijumaa Desemba 14, Katibu Tawala wa Mkoa, Jumanne Sagini, amesema sababu kubwa iliyofanya wanafunzi wengi kushindwa kuchaguliwa ni kutokana na kuwepo kwa changamoto ya ukosefu wa vyumba vya madarasa.

Sagini amesema mkoa mzima unahitaji vyumba vya madarasa 312 ili kuwapokea wanafunzi hao ambao hawakupata nafasi katika awamu ya kwanza ya uchaguzi, na kuongeza kuwa juhudi zinahitajika ili madarasa hayo kujengwa na wanafunzi hao kuanza masomo.

“Halmshauri ya Wilaya ya Busega wanahitaji vyumba vya madarasa 84, Bariadi vijijini vyumba 71, Maswa 68, Itilima 39,Bariadi Mji 29 na Meatu vyumba 21 hadi kufikia Februari 15, mwakani ujenzi wa vyumba hivi uwe umekamilika na wanafunzi hawa waanze shule haraka,” amesemaSagini.

Aidha, amewataka wananchi, viongozi wa kisiasa, watendaji wa halmashauri kuhakikisha vyumba hivyo vinajengwa huku akiwataka wazazi wa wanafunzi waliokosa nafasi kuwa wavumilivu.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,549FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles