25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

UPOFU: TATIZO LINALOWAKABILI ZAIDI WATOTO WA KIAFRIKA

young-girl-in-pink-glasses

Na Mwandishi Wetu,

KWA mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kila dakika, kuna mahali duniani ambapo mtoto anapata upofu.

Ukanda wa Afrika katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara ni ukanda wenye maambukizi makubwa ya upofu kwa watoto duniani ambao uwiano wake ni 1.24 kwa kila watoto 1,000; tofauti na uwiano wa 0.8 nchini India huku Ulaya ikiwa ni uwiano wa 0.3.

 Sababu za upofu kwa watoto

Mkurugenzi Mtendaji wa Afrika wa Shirika la Kimataifa la Kuzuia Upofu (IAPB) na mwanachama wa Kamati ya Muda ya Afrika (ORBIS), Dk. Daniel Etya’ale

anasema katika mataifa ya Afrika Mashariki kama Kenya na Uganda, sababu kuu ya upofu kwa watoto huwa ni mtoto wa jicho.

Dk. Daniel ambaye shirika lake limefanya kazi katika nchi 88 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1982, ikiwa ni pamoja na kuanzisha kliniki 28 za kutoa huduma za macho kwa watoto nchini India tangu mwaka 2007.

Anasema kuwa watoto wenye upofu Kusini mwa Jangwa la Sahara wanakabiliwa na changamoto kubwa.

“Kwanza, wengi hawafikiwi kiurahisi kwa ajili ya kupatiwa tiba sahihi; pili ni rahisi kwao kupata athari kubwa, karibu nusu yao wana uwezekano wa kufariki dunia miaka miwili hadi mitatu baada ya kuwa vipofu,” anasema Dk. Daniel.

Anabainisha kuwa kiasi kikubwa cha vifo kwa watoto wenye upofu kinaweza kuhusishwa na mazingira ya kitabibu ambayo yanasababisha upofu wao.

“Mtoto wa jicho, kwa mfano, inasababishwa na kukosekana kwa vitamini A ambayo pia inasababisha kupungua kwa uwezo wa kupambana na maambukizi,” anasema.

WHO inapendekeza kituo kimoja cha kutibu magonjwa ya macho kwa watoto katika kila penye watu milioni kumi. Lakini vituo hivyo ni vichache mno katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara huku nchi ya Afrika Kusini ikiwa na kituo kimoja cha aina hiyo katika Hospitali ya Watoto ya Shirika la Msalaba Mwekundu mjini Cape Town.

“Mataifa mengine 11 yanaweza kuwa na aina fulani ya vituo vya kutoa huduma ya macho kwa watoto,” anasema.

Profesa Colin Cook, ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Macho katika Chuo Kikuu cha Cape Town na wa Hospitali ya Msalaba Mwekundu, anasema hatua za kuzuia upofu kwa watoto zinatofautiana kati ya kanda moja na nyingine na kwamba wakati mwingine unahitaji kufanyiwa upasuaji.

Anasema kuna wakati watoto wanahitaji miwani, au hata huduma za kijamii na zile za afya ya msingi kama vile kupatiwa chanjo na kuboresha lishe.
Mtoto wa jicho pia imehusishwa na ugonjwa wa watoto wa rubella ambao huambukiza kwa kasi kubwa na umechangia kwa kiasi kikubwa watoto kuwa na mtoto wa jicho nchini Afrika Kusini, Zambia na Kenya… ili kukabiliana nao, programu za chanjo zimeimarishwa kuhakikisha kuwa wasichana wanachanjwa dhidi ya ugonjwa huo kabla hawajafikia umri wa kujifungua.

Kugundua mapema na kuzuia matatizo ya macho kwa watoto kunahitaji mfumo shirikishi zaidi.
ORBIS inatumia baadhi ya hatua kama vile Flying Eye Hospital, hospitali ya kutoa mafunzo ya magonjwa ya macho inayohama ndani ya ndege ya DC-10 na Cyber-Sight – utoaji wa mafunzo ya tiba kwa njia ya mtandao.

Dk. Hunter Cherwek ni Mkuruegnzi wa Tiba wa Hospitali ya Flying Eye, anasema kama watoto watapima kila macho, kutasaidia kupunguza tatizo hili.

“Kupima macho shuleni ni muhimu, lakini maeneo mengi tunayokwenda hakuna utaratibu huu, hata kwa ajili ya kupatiwa miwani,” anasema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles