22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Upinzani wamkataa mtoto wa rais Chad

N’Djamena, Chad

Baada ya kifo cha Rais wa Chad, Idriss Deby, jeshi la nchi hiyo limemteua mtoto wake kushika wadhifa huo, uamuzi ambao sasa unapingwa na wanasiasa wa upinzani.

Deby mwenye umri wa miaka 68, ambaye aliiongoza Chad kwa miaka 30, amefariki baada ya kupigwa risasi wakati akiliongoza jeshi kukabiliana na waasi.

Huku mtoto wake, Mahamat Idriss Deby, akitarajiwa kuongoza kwa miezi 18 iliyobaki kabla ya uchaguzi, wapinzani wamesema nchi hiyo haiendeshwi kwa kurithishana.

Chad inaomboleza kifo cha rais wa nchi hiyo aliyefariki dunia Jumatatu Aprili 19 kutokana na majeraha aliyoyapata alipokua akiongoza mapigano dhidi ya waasi wa FACT.

Kifo cha Rais wa Chad Idriss Déby Itno kilitangazwa Jumanne Aprili 20 na Baraza la Jeshi la Mpito (CMT). Wakati huo huo, liliitangaza kusimamishwa kwa Katiba na vile vile kuvunjika kwa serikali na Bunge. Spika wa Bunge anasadikiwa kuwa alikataa kukaimu nafasi hiyo.

Tayari serikali imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku nne kuanzia jana Jumaanne. Idriss Deby atazikwa siku ya Ijumaa.

Jeshi lagawanyika

Suala la ukabila limeanza kujitokea katika Baraza hilo la mpito wengi wakiona kuwa wengi katika kundi la maafisa wa ngazi ya juu wanaounga mkono mwanae Idriss Deby, Mahamat Mahamat Idriss Déby Itno, nikutoka upande wa Kaskazini anakotoka hayati Deby.

Jeshi limesema Baraza la Mpito tayari limeundwa na litaiongoza nchi hiyo kwa muda wa miezi 18 kabla ya kuitishwa uchaguzi mkuu. Baraza hilo linaongozwa na mtoto wa hayati rais Deby aitwaye Mahammat na jeshi limewatolea wito raia wa Chad kuimarisha amani, uthabiti na utii wa sheria katika kipindi chote cha msiba wa taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,208FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles