UPINZANI KUWASILISHA BAJETI YA KURASA 200

0
538

Na Kulwa Mzee-Dodoma

KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni, imesema bajeti yao ya mwaka 2017/18 ni ya  historia ina kurasa 200  ikiwa na makadirio ya Sh trilioni 29.9.

Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, Halima Mdee, alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mapendekezo ya bajeti ya Serikali mwaka 2017/18 iliyowasilishwa wiki na Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango.

“Bajeti ya kambi ya upinzani, itakuwa na kurasa nyingi kutokana na kuongezeka kwa matatizo, itawasilishwa kesho(leo) na Mbunge wa Mbozi, David Silinde ambaye ni Naibu Waziri Kivuli wa wizara hiyo, sijui kama wataweka mwongozo kuhusu mzigo huu au vipi,”alisema.

“Bajeti iliyowasilishwa Juni, 8 mwaka huu ina upungufu mkubwa, imelenga kumnyonya mwananchi masikini.

“Katika bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/18, takwimu za vitabu vyake vya mapato na matumizi zinatofautiana, kitabu cha mapato kinaonyesha kwa mwaka itakusanya Sh trilioni 23.9, kitabu cha matumizi kinaonyesha inakusudia kutumia Sh trilioni 26.9, ikiwa ni ongezeko la Sh trilioni 3, wakati huo huo sura ya bajeti inaonyesha bajeti kwa mwaka 2017/18 ni Sh trilioni 31.7.

“Kambi rasmi ya upinzani bungeni inaungana na wale waliosema bajeti hii ni ya ajabu maana haijawahi kutokea kukawa na mkanganyiko mkubwa namna hii wa takwimu katika bajeti,”alisema.

Alisema makadirio ya bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani ni Sh trilioni 29.9 ambako vipaumbele vyao ni   sekta ya elimu iliyotengewa asilimia 20, viwanda asilimia 15, nishati asilimia 15, kilimo asilimia 10 na sekta nyingine zitapata asilimia 40 iliyobakia.

Alitaja vyanzo vipya vya mapato kuwa ni mapato yanayotokana na uvuvi katika bahari kuu Sh bilioni 492.1, sekta ya madini Sh bilioni 5.59, kodi ya mrabaha na payee Sh bilioni 270, kupunguza misamaha ya kodi kuwa asilimia moja ya pato la taifa Sh bilioni 145.2 sawa na  Euro trilioni 2.2.

Alisema mapato kutoka sekta ya utalii, Sh bilioni 592.7 na sekta ya michezo ya kubahatisha Sh bilioni 30 ambako jumla ya vyanzo vya mapato ya nyongeza ni Sh trilioni 3.7.

“Vipaumbele hivi vikitekelezwa kwa ukamilifu Tanzania tutapunguza umasikini kwa asilimia 50 kwa kuwa ni vipaumbele vitakavyochochea ajira kwa watu wengi,” alisema.

Kuhusu bajeti iliyowasilishwa na Waziri Mpango, Mdee alisema ilipotangazwa kuondolewa  kodi ya ada ya mwaka ya ‘Motor Vehicle’ magari, viongozi wengi walifurahia bungeni.

“Sisi viongozi wa siasa tuna madeni mengi viporo kutokana na kuwa na magari mengi yanayodaiwa kwa sababu hatulipi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here