28.6 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

UPINZANI KUANZISHA UWAZIRI MKUU KENYA

NAIROBI, KENYA


VIONGOZI wa muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya (NASA) wamesaini makubaliano ya kugawana madaraka huku wakibuni cheo cha uwaziri mkuu.

Makubaliano hayo yatawaunganisha dhidi ya chama tawala cha Jubilee katika uchaguzi mkuu ujao.

Viongozi hao wamekubaliana cheo cha uwaziri mkuu kiende kwa mtangaza nia atakayeibuka wa tatu katika mchujo wa uteuzi wa mgombea urais wa muungano huo.

Kwa mujibu ya vyanzo vya habari kutoka mkutano uliofikia makubaliano hayo juzi, mgombea atakayeshinda uteuzi huo atapeperusha bendera ya chama hicho, wa pili atakuwa naibu wa rais.

Makubaliano hayo pia yanamtaka rais atakayechaguliwa kutumia uwezo wake kubuni wadhifa wa Waziri Kiongozi.

Muungano huo baadaye utafanya mabadiliko ya kikatiba ili kubadilisha ofisi ya waziri huyo kuwa ile ya Waziri Mkuu kama ilivyokuwa katika serikali ya umoja wa kitaifa ya 2008-2013.

Viongozi wakuu wa muungano huo ni Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga (ODM), Makamu wa Rais wa zamani Kalonzo Musyoka (Wiper),  Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Moses Wetangula (Ford Kenya) na Naibu Waziri Mkuu wa zamani Musalia Mudavadi (ANC).

Nyadhifa nyingine zilizotajwa katika makubaliano hayo ni pamoja ni Spika wa Seneti, Kiongozi wa wengi katika Bunge la Seneti na Kiongozi wa wengi katika Bunge la uwakilishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles