23.2 C
Dar es Salaam
Monday, February 6, 2023

Contact us: [email protected]

Upinzani dhidi ya Netanyahu waundwa

TEL AVIV, ISRAEL

WANASIASA wawili wa mrengo wa kati, kiongozi wa zamani wa vikosi vya wanajeshi, Benny Ganz na mkuu wa chama cha Yesh Atid, Yair Lapid, wametangaza kuunganisha vyama vyao kwa lengo la kushindana na Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu, uchaguzi mkuu utakaoitishwa Aprili 19.

Kwa mujibu wa Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani, viongozi hao wamekubaliana kubadilishana zamu ya waziri mkuu baada ya kila mmoja kutumikia miaka miwili na nusu.

Taarifa ya pamoja iliyochapishwa na viongozi hao wawili, inasema: “Jukumu lao kuelekea usalama wa taifa ndiyo sababu ya kuamua kuungana ili kubuni chama kipya tawala nchini Israel. Tunaweza kumng’oa madarakani Netanyahu. Kuna fursa ya kihistoria iliyojitokeza kubadilisha kipaumbele cha taifa,” amesema Lapid.

Kiongozi huyo ameongeza kusema na kuyataja masuala ya kudhamini usalama, kupambana na ughali wa maisha, kuunusuru mfumo wa bima ya afya na kufufua juhudi za kidiplomasia. Kiongozi mwingine wa zamani wa jeshi, Gabi Ashkenazi, amejiunga pia na muungano huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles