23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Upelelezi wanafunzi wanaotuhumiwa kuua mwenzao haujakamilika

Nyemo Malecela -Kagera

KESI ya mauaji inayowakabili wanafunzi wa Shule ya Sekondari Katoro Islamic ya mkoani Kagera, wanaotuhumiwa katika mauaji ya mwanafunzi mwenzao, Mudy Muswadiku, imeharishwa hadi Novemba 11 kutokana na upelelezi kutokamilika.


Kesi hiyo namba 18/2019 inayosikilizwa na Hakimu Frola Kaijage, ilitajwa jana Mahakama ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera ambako Wakili wa Serikali, Juma Mahona alisema upelelezi wa kesi hiyo unakaribia mwishoni.


Alisema watuhumiwa hao wakiwa gerezani hivi karibuni walitembelewa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa (RCO) ambaye alisema shauri lao liko katika hatua ya mwisho.


“Kwa utaratibu wa makosa ya namna hii, RCO anapokamilisha upande wake analeta jalada kwetu na likishafika tunalipitia ili kuandaa nyaraka kwa ajili ya kupeleka shauri hilo Mahakama Kuu.


“Tumeambiwa watuhumiwa wawe wavumilivu, taratibu hizo zitakapokamilika watajulishwa na kupeleka nyaraka Mahakama Kuu na zikitoka Mahakama Kuu na kurudi Mahakama ya Wilaya hapo ndipo upelelezi utakuwa umekamilika,” alisema.


Kwa upande wa watuhumiwa waliokuwa wakisoma kidato cha nne kufanya mitihani wa taifa unaotarajia kuanza Novemba 4, Mahona alisema hawezi kuzungumzia suala hilo maana watuhumiwa waliiomba mahakama iwaruhusu kufanya mtihani huo.
“Waliiomba mahakama, wa kulizungumzia suala hilo ni mahakama yenyewe,” alisema.


Watuhumiwa katika kesi ya mauaji ya mwanafunzi Mudy aliyekuwa anasoma kidato cha nne ni Sharifu Amri (19), Fahadi Abdulazizi Kamaga (20), Husama Ramadhan (17), Sharifu Huled (19), Abdalah Juma (19), Hussein Mussa (20), mwalimu Majaliwa Abud (35) na Badru Tibagililwa (27) ambaye ni mlinzi.


Mauaji hayo yalitokea Aprili 14, katika shule hiyo iliyopo Halmashauri ya Bukoba Vijijini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles