26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

UPELELEZI ‘NDAMA MTOTO WA NG’OMBE’ WAKWAMA

Na KULWA MZEE-DAR ES SALAAM               |                 


UPELELEZI wa kesi inayomkabili mfanyabiashara , Ndama Shabani Hussein maarufu kama Pedeshee Ndama Mtoto ya Ng’ombe, umekwama kukamilika kwa sababu Jamhuri inasubiri upelelezi kutoka Australia.

Hayo yalibainika jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde wakati kesi hiyo ilipokuwa inatajwa.

Akiiwakilisha Jamhuri, Wakili wa Serikali, Elia Athanas alidai   upelelezi wa kesi hiyo  haujakamilika,  kwamba kuna taratibu baina ya nchi mbili Tanzania na Australia bado unaendelea ili kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo.

Athanas aliomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa  kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Wakili wa utetezi, Nashon Nkungu alisema anasikitika   upande wa mashtaka haulipi uzito suala hilo na kwamba inashangaza upelelezi  haukamiliki kwa zaidi ya mwaka sasa.

Nkungu aliiomba mahakama kuangalia kesi hiyo kwa jicho la tatu ambalo ni kutenda haki.

Aliiomba upande wa mashtaka uonywe na kutekeleza jukumu lake katika kesi hiyo ikiwa Jamhuri imeshindwa kukamilisha upelelezi suala hilo lifanywe kama sheria inavyotaka ,  hati ya mashtaka iondolewe.

Wakili Athanas baada ya kusikiliza hoja hizo za upande wa utetezi alisisitiza kuwa suala hilo linahusisha nchi mbili tofauti.

“Sisi kwa upande wetu tumekamilisha bado upande huo mwingine kwa kuwa wao wana utaratibu wao na hatuwezi kuwalazimisha watujibu.

“Tunaomba wawe wavumilivu kwa sababu siyo nia ya Jamhuri kuchelewesha shauri hilo,” alidai.

Baada ya kusikiliza hoja zote hizo, Hakimu Kasonde alisema “hakuna ubishi suala la upelelezi linahusisha nchi mbili, tuwape nafasi”  na kuiahirisha kesi hadi Septemba 21, mwaka huu.

Ndama ambaye kwa sasa yupo nje kwa dhamana,  anakabiliwa na shtaka la kwanza hadi la tano baada ya kulikubali shtaka la sita la kutakatisha fedha, kuhukumiwa na kuachiwa huru baada ya kulipa faini ya Sh milioni 200 na kukwepa kesi kifungo cha miaka mitano jela.

Ndama kwa sasa anakabiliwa na mashtaka matano ya  kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Miongoni mwa mashtaka yanayoendelea kumkabili ni kuwa  Ndama anadaiwa Februari 20, 2014 Dar es Salaam, alighushi nyaraka ya kibali cha kusafirisha madini na sampuli za madini kwa kusudi la kuonyesha kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited.

Pia kampuni hiyo  iliruhusiwa kusafirisha makasha manne ya dhahabu yenye kilogramu 207 yenye thamani ya Dola za Marekani 8,280,000.00 kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited wakati akijua si kweli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles