23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

UPELELEZI KESI YA MDEE WAKAMILIKA

Upelelezi wa kesi ya kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais Dk John Magufuli inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee umekamilika.

Hayo yalidaiwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa wakati kesi hiyo ilipokuwa ikitajwa leo Septemba 12.

“Mheshimiwa hakimu, upelelezi wa kesi hii umekamilika, upande wa jamhuri tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali,” alidai Wakili wa Serikali Mkuu, Mutalemwa Kishenyi.

Mahakama ilikubali maombi hayo na kuahirisha kesi hadi Oktoba 11 mwaka huu kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Katika kesi hiyo, Halima anadaiwa  kutenda kosa Julai 4, mwaka huu katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa Wilaya ya Kinondoni.

Anadaiwa  kumtukana Rais Magufuli  kwa kusema “anaongea hovyo hovyo, anatakiwa  afungwe breki” kitendo ambacho kingeweza  kusababisha uvunjifu wa amani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles