UPELELEZI KESI YA MALINZI WAKAMILIKA

0
578

Na Mwandishi wetu    |

UPELELEZI wa kesi ya aliyekuwa Rais wa TFF,  Jamal Malinzi, Katibu Mkuu wake Mwesigwa Celestine na mhasibu Nsiande Mwanga umekamilika.

Hayo yalibainishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Wakili wa Serikali kutoka Takukuru, Leonard Swai alidai kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi umekamilika wanaomba tarehe ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.

Mahakama imepanga kusikiliza maelezo ya awali Aprili 11 mwaka huu.

Washtakiwa hao wanaokabiliwa na mashtaka 28 yakiwemo ya utakatishaji fedha wa Dola za Marekani 375,418 ambayo yanawafanya wasote mahabusu kutokana na kutokuwa na dhamana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here