30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Upelelezi kesi ya dada wa Balali upo hatua za mwisho – Wakili

Kulwa Mzee, Dar es salaam

DADA wa aliyekuwa Gavana wa Banki Kuu, marehemu Daudi Balali, Elizabeth Balali (54) anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, anaendelea kusota rumande huku ikielezwa upelelezi uko katika hatua za mwisho.

Kesi hiyo ilikuja jana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kutajwa.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Simon Wankyo, alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Vick Mwaikambo kwamba kesi ilikuja kwa kutajwa na upelelezi unaendelea katika hatua za mwisho.

Alidai Hakimu Mfawidhi, Godfrey Isaya anayesikiliza kesi hiyo ana udhuru, hivyo aliomba ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Mwaikambo aliiahirisha kesi hiyo hadi Februari 26, kwa kutajwa na mshtakiwa amerudishwa rumande.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kati ya Oktoba 19 na Desemba 21, 2017 Dar es Salaam, alijipatia Sh milioni 25  kutoka kwa Dk. Roderick Kisenge kwa ulaghai.

Inadaiwa alijipatia fedha hizo baada ya kujifanya anamuuzia eneo la mita za mraba 900 ambazo halijapimwa lililopo Boko Dovya, Kinondoni wakati akijua eneo hilo si lake.

Katika mashtaka ya utakatishaji fedha, inadaiwa kuwa katika kipindi hicho mshitakiwa huyo alipokea kiasi hicho cha Sh milioni 25 kutoka kwa Dk. Kisenge kupitia akaunti yake iliyopo Benki ya CRDB wakati akijua fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Elizabeth hakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles