32.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 5, 2024

Contact us: [email protected]

Upelelezi kesi wathamini madini haujakamilika

Na NORA DAMIAN – DAR ES SALAAM



UPELELEZI wa kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wawili wa serikali, wathamini wa madini ya almasi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  haujakamilika.

Jana, kesi hiyo ilitajwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali, Tulia Helela, aliyedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa upelelezi  haujakamilika.

Alidai  jalada la kesi hiyo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na kuomba ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Mashauri alisema kesi hiyo ni ya muda mrefu kwa sababu  jalada lilikuwa kwa DPP likapelekwa kwa DCI na likarejeshwa kwa DPP, Juni 18 mwaka huu.

Aliutaka upande wa mashitaka kuwatendea haki washtakiwa.

Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 5, mwaka huu itakapotajwa tena kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika.

Washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania  (Tansort), Archard Kalugendo na Mthamini Almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu ambao ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na Madini.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wakidaiwa kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 2.4.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31, 2017 katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Shinyanga.

Washtakiwa hao wanadaiwa kwa pamoja wakiwa wathaminishaji wa almasi wa serikali na waajiriwa wa wizara hiyo, waliisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 1,118,291.43.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles