30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Upelelezi kesi bosi wa OBC wakaribia kukamilika

Na JANETH MUSHI

UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi na kusababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 12.4, inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya Otterlo Business Limited (OBC), Isaya Mollel, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuwa upelelezi uko katika hatua za mwisho.

Jana mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Gwantwa Mwankuga, upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili Ahmed Khatibu na Hellen Osujaki (Takukuru) huku Mollel akiwakilishwa na mawakili Daudi Haraka, Goodluck Peter, Valentine Nyalu na Elvaison Maro.

Wakili Khatibu alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilipangwa kutajwa na kuwa Jamhuri wako katika hatua za mwisho kukamilisha upelelezi wake na kuomba mahakama hiyo kuiahirisha na kuipangia tarehe nyingine.

Upande wa utetezi wakiongozwa na wakili Maro, walikubaliana na hoja hiyo na kuieleza mahakama kuwa wanahifadhi hoja zao hadi hapo upande wa Jamhuri watakapokuwa wamekamilisha upelelezi ndipo wataziwasilisha.

Hakimu Mwankuga alikubaliana na pande zote mbili na kuahirisha shauri hilo hadi Desemba 4 litakapotajwa tena.

Awali Novemba 7, mwaka huu, kesi hiyo iliahirishwa kwa madai kuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Martha Mahumbuga, anayepaswa kuisikiliza hakuwepo mahakamani.

Aidha Oktoba 25, mwaka huu kesi hiyo iliahirishwa na kwamba madai mwafaka baina ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) na mawakili wa Mollel haujafikiwa.

Oktoba 15 mwaka huu, shauri hilo lilipotajwa mahakamani hapo, wakili wake alidai Mollel amemwandikia barua DPP kuomba kukiri mashtaka 10 yaliyokuwa yanamkabili awali, yakiwemo ya utakatishaji fedha haramu, kukwepa kodi na kusababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 2.8 katika kesi ya awali.

Katika kesi hiyo, moja ya mashtaka yanayomkabili Mollel ni kusababisha hasara ambapo ilidaiwa kati ya Januari 2010 na Aprili 2018 akiwa katika mikoa ya Kilimanjaro, Dar es Salaam na Arusha, aliwasilisha nyaraka za uongo, kushindwa kulipa kodi mbalimbali za Serikali, aliisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 12.4.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles