26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Upatikanaji taulo za kike vijijini utasaidia masomo

 AMINA OMARI MKINGA

IMEELEZWA taulo za kike (pads), iwapo zitapatikana kwa uhakika kwenye shule hasa maeneo ya vijijini, zitaongeza mahudhurio ya wanafunzi wa kike.

Hayo yalielezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Mkinga, Rashid Gembe wakati wa utambulisho wa mradi wa hedhi salama unaofadhiliwa na mtandao wa watu wanaoishi na virus vya UKIMWI SHDEPHA kwa wakuu wa idara za maendeleo ya jamii na maofisa elimu msingi na sekondari wilayani humo.

Alisema imekuwa nichangamoto kubwa kwa watoto 

 wanaotoka familia duni kupata vifaa hivyo, hali inayosababisha kutohudhuria masomo kwa wakati.

“Tunaamini upatikanaji wa taulo hizi katika shule zetu, utakuwa mwarobaini wa changamoto ya utoro kwa watoto wa kike, hivyo kupata fursa ya kuhudhuria masomo bila ya vikwanzo,”alisema.

Mratibu wa Mtandao huo, Marium Kamote aliziomba halmashauri kutenga bajeti ndogo kupitia mapato yao ya ndani ambayo itaweza kutumika kununua pedi kwa ajili ya kuziweka katika shule.

Alisema Serikali na jamii, vinajukumu la kuhakikisha lina mlinda mtoto wa kike kwa kuhakikisha anakuwa na hedhi 

 salama na kumuepusha na vikwanzo vinavyomzua kutimiza lengo lake .

“Tungependa kuona halmashauri inatenga bajeti ndogo kwa ajili ya kumsaidia mtoto wa kike kuboresha mazingira yake ya kupata elimu na hedhi haiwi kikwazo cha kushindwa kufikia malengo yake”alisema.

Ofisa Mradi Hedhi Salama, Devotha Mbenna alisema mradi unatarajiwa kuwepo wilaya tano za mkoa huo kwa ajili ya kujenga uelewa kuhusu hedhi salama.

Alisema wanatarajia elimu ya hedhi salama kufika kwa wanafunzi wa kike na wakiume ili waweze kuona hedhi ni jambo la kawaida tuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles