24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

UPATIKANAJI DAWA WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 81

Na HAMISA MAGANGA

-DAR E SALAAM

UPATIKANAJI wa dawa katika hospitali na vituo vya afya nchini umeongezeka kutoka asilimia 51 mwaka jana hadi kufikia asilimia 81, mwaka huu.

Akifanya majadiliano na wahariri wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Sikika, Irenei Kiria, alisema kwa ujumla hali ya upatikanaji wa dawa nchini inaanza kuimarika ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Alisema hali hiyo inatokana na vituo vya kutolea huduma kuruhusiwa kununua dawa kutoka kwa wauzaji binafsi pindi zinapokosekana katika Bohari ya Dawa (MSD).

“Kwa miaka kadhaa tumekuwa tukiishauri Serikali iondoe ukiritimba wa MSD kuwa sehemu pekee ya hospitali na vituo vya afya kununulia dawa kwa kuwa ndio chanzo cha kuadimika kwa dawa, kwani zikikosekana huko basi na sehemu za kutolea huduma zinakosa dawa.

“Sasa hivi vituo vimeruhusiwa kununua kutoka kwa wauzaji binafsi na hali ya upatikanaji wa dawa imekuwa nzuri,” alisema Irenei.

Alitoa mfano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, licha ya kununua dawa kutoka MSD, pia huagiza wenyewe nje ya nchi ikiwamo India na kwa wauzaji wa ndani.

Alisema licha ya dawa kupatikana kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa awali, gharama nazo zimeshuka kwa kiasi kikubwa.

Taarifa ya bei ya dawa iliyotolewa na MSD hivi karibuni, inaonyesha bei zimeshuka kati ya asilimia 15 hadi 80, jambo ambalo ni faraja kwa wananchi.

Hata hivyo, alisema pamoja na maboresho yaliyofanyika, kitendo cha MSD kuwa mnunuzi na msambazaji pekee wa dawa bado ni changamoto, kwa kuwa nchi ni kubwa kijiografia na vituo vya kutoa huduma ni vingi.

Baadhi ya wahariri waliokuwapo katika majadiliano hayo, walipongeza hatua hiyo, lakini wakashauri upatikanaji huo wa dawa unapaswa kwenda sambamba na rasilimali watu, kwa kuwa katika baadhi ya vituo vya afya nchini hakuna madaktari wa kutosha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles