27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

UPASUAJI WA MASIKIO KUFANYIKA NCHINI

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na mzazi wa mtoto Melkizedek Kibona, ambaye amefanyiwa upasuaji wa kupandikizwa kifaa cha usikivu (Cochlea Implant) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, huduma hiyo imeanza kutolewa kwa mara ya kwanza katika hospitali hiyo. Picha na Veronica Romwald.

 

 

NA VERONICA ROMWALD -DAR ES SALAAM

SERIKALI imesitisha ufadhili na rufaa za matibabu nje ya nchi kwa wagonjwa wanaohitaji huduma ya kupandikizwa vifaa vya usikivu kuanzia sasa.

Hayo yalielezwa Dar es Salaam jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alipokuwa akizindua huduma ya upandikizaji vifaa hivyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Alisema Serikali itaendelea kufuta rufaa za matibabu nje ya nchi, hata kwa huduma ya upandikizaji figo inayotarajiwa kuanza kutolewa hospitalini hapo Julai.

Alisema kila mwaka Serikali ilikuwa ikitumia kati ya Sh bilioni 1.2 hadi 1.4 kufadhili matibabu hayo yaliyokuwa yakitolewa kwa watoto waliozaliwa na matatizo hayo.

“Hizi ni fedha nyingi mno ambazo zilikuwa zikitumika kugharamia matibabu ya watoto ambao tulikuwa tukiwapeleka nje ya nchi kutibiwa.

“Wagonjwa ambao watahitaji matibabu ya kibingwa zaidi tutaleta wataalamu kutoka nje ya nchi waje wawafanyie upasuaji hapa hapa, tutafanya kambi za upasuaji, lakini ikiwa mtu atataka kwenda nje itampasa agharamie matibabu mwenyewe,” alisema.

Waziri Ummy alisema kuanzishwa kwa huduma hiyo nchini kutawezesha wagonjwa wengi kupata huduma hiyo tofauti na ilivyokuwa awali.

“Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kati ya watoto 1,000 wanaozaliwa inakadiriwa wawili au watatu huzaliwa na tatizo la usikivu. Hapa nchini inakadiriwa kila mwaka watoto 200 huzaliwa wakiwa na tatizo hili.

“Uwezo wa kusaidia upasuaji huu kila mwaka ilikuwa watoto 15 pekee ndiyo wananufaika na ufadhili, maana yake watoto 185 kila mwaka wanabaki wakiwa na tatizo.

“Takwimu za MNH zinaonyesha asilimia 95 huhitaji kufanyiwa upasuaji huu, kila mtoto mmoja gharama ilikuwa kati ya Sh milioni 80 hadi 100, kwa kuwa huduma inaanza kutolewa Muhimbili, mtoto mmoja itatugharimu Sh milioni 36.9 hii ni sawa na punguzo la asilimia 60,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles