23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Upasuaji kidole tumbo, mafindofindo unaongeza uzazi  

MIMBANa Mwandishi Wetu  

UTAFITI umebaini kuwa wanawake ambao wametolewa kidole tumbo ama ‘appendix’ au kutolewa kifindofindo au kifuko ama ‘tonsils’ kwa njia ya upasuaji wanapata uwezo mkubwa zaidi wa kushika mimba.

Utafiti huo wa miaka 15, uliofanywa katika Chuo Kikuu cha Dundee, ulihusisha uchunguzi wa rekodi za matibabu ya zaidi ya wanawake nusu milioni wa nchini Uingereza.

Utafitu huu unawapa akina mama wanaotafuta ujauzito afueni kubwa mno pia kuwaondolea wasiwasi kuhusu uoga wa kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa kidole tumbo yaani appendix kwamba itahitilafiana na uwezo wao wa kupata ujauzito.

Utafiti huo pia ulifanywa kwa wanawake nusu milioni waliofanyiwa upasuaji wa kuondolewa mafindofindo kwa lugha ya Kiingereza tonsils, kama kweli inaleta utasa miongoni mwa wanawake.

Mmoja wa watafiti hao, Daktari Sami Shimi, anasema madakatari wengi walipotoshwa walipokuwa chuoni wakisomea udakatari.

”Chuoni tulielezwa kuwa kufanyiwa oparesheni ya kuondolewa kidole tumbo inasababisha utasa na kumfanya mwanamke asiweze kupata ujauzito,” anasema.

Mtafiti huyo anasema kuwa oparesheni ya kuondoa mafindofindo au hata kuondoa kidole tumbo, haisababishi utasa.

Daktari Sami anasema utafiti huu unawahakikikishia wasichana kwamba wakiwa na matatizo ya ‘appendix’ au kidole tumbo wasiwe na wasiwasi kwamba itapunguza uwezo wao wa kupata ujauzito siku za baadae.

Mwanasayansi huyo wa maumbile anasema badala yake kufanyiwa upasuaji wa kuondoa sehemu hizo za mwili zikiwa zinauma au kutatiza au hata zikiwa zinapata maambukizi ya mara kwa mara inamuongezea mwanamke uwezo wa kujaliwa kupata mimba.

Utafiti huo  pia ulihusisha uchunguzi wa rekodi za matibabu ya zaidi ya wanawake nusu milioni wa Uingereza.

Wanasayansi hawa wanaujumbe maalumu tena wa matumaini kwa akina mama.

Nao wanasema pengine tatizo lako la kutoweza kuzaa wewe mama linasababishwa na matatizo ya kidole tumbo yaani au huenda unamatatizo ya muda mrefu ya mafindofindo.

Sasa basi, wanashauri kufika haraka hospitalini kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa vitu hivyo ili kujiongezea uwezo wa wa kupata ujauzito na kujaaliwa watoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles