23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Unywaji maziwa huzuia maumivu ya misuli

Amina Omari,TANGA

IMEELEZWA unywaji wa maziwa kwa watu wenye umri mkubwa  huzuia maumivu ya misuli na kurudisha ute ulipotea kwenye misuli .

Hayo yamesemwa na Meneja Vyanzo vya Maziwa wa Kiwanda cha kuzalisha maziwa cha Tanga Fresh, Annadomana Nyanga wakati akizungumza na  waandishi wa habari na watafiti waliokuwa  katika mafunzo ya habari za kisayansi yaliyoendeshwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia ..

Alisema  tafiti zinaonyesha maziwa yana wingi wa madini ya proteni ambayo yanasaidia kuimarisha mifupa hasa kwa watoto na wazee.

Alisema  iwapo wazee  watakunywa maziwa katika kiwango stahiki, wataepukana na uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya mifupa ambao umekuwa changamoto kubwa kwao.

“Tatizo kubwa lililopo,Watanzania hatuna utamaduni wa kunywa maziwa, takwimu zinaonyesha mtu mmoja anastahili kunywa lita 100 kwa mwaka,mpaka sasa  Watanzania wanakunywa lita 47 pekee kwa mwaka,”alisema Nyanga.

Alisema sasa wapo kwenye mpango wa kuwaelimisha wafugaji namna bora ya ufugaji bora ambao utawezesha kuongeza uzalishaji.

Alisema ili kufanikisha hilo, tayari wameshaanza ushirikiano na Kituo cha Utafiti wa Mifugo (TALIRI- Tanga) ili kuzalisha malisho bora.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa  TALIRI kituo cha Tanga,  Zablon Nziku alisema kwa kutumia teknolojia mpya yauzalishaji wanauhakika watamaliza changamoto ya malisho kwa wafugaji.

Alisema  kikwazo kikubwa cha wafugaji kutoendelea ni kutokana na ukosefu wa malisho ya uhakika, hasa kipindi cha kiangazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles